MAMBO YAPAMBA MOTO ZIARA YA MAGWIJI WA REAL MADRID NCHINI
Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
WAZEE
wa kale walishasema, `Bahati haiji mara mbili`!. Kumekucha kwa
Watanzania kuwaona `laivu` magwiji waliotikisha soka la dunia ngazi ya
klabu na michuano ya kimataifa ikiwemo kombe la dunia.
Magwiji
waliocheza kwa mafanikio makubwa katika klabu ya Real Madrid
wanatarajia kufanya ziara ya siku nne nchini kuanzia Agosti 22 mwaka huu
ambapo watacheza mechi moja ya kirafiki dhidi ya kikosi maalum cha
nyota wa Tanzania.
Ziara
hiyo ni mwaliko wa kampuni ya Tanzania Sisi ni Nyumbani (TSN), chini ya
mkurugenzi wake mkuu, Farough Baghozah na meneja wa ziara hiyo ni
Dennis Ssebo.
Akizungumza
na mtandao huu mchana wa leo, Dennis Ssebo amesema maandalizi ya ziara
hiyo yanakwenda vizuri na watanzania watarajie kuwaona wachezaji wakubwa
waliotamba miaka ya nyuma kama vile Ronaldo Delima, Luis Figo, Roberto
Carlos, Zinedine Zidane na wengineo.
“Ninaloweza
Kusema ni kwamba, Watanzania wakae tayari kupokea wachezaji 27 wa
zamani wa timu ya Real Madrid na mashabiki 23 kutoka Hispania wanaokuja
kuwashangilia magwiji wao. Kwahiyo jumla tunapokea watu 50 kutoka
Hispania kwa ajili ya ziara hii”. Alisema Ssebo.
“Ni
ziara ambayo tulifikiria itakuwa fupi, lakini wenzetu kumbe wameipenda
nchi na wanaifahamu, kwahiyo ni ziara ambayo itachukua takribani siku
nne”. Aliongeza.
Ssebo
alisema Magwiji hao wataingia nchini Agosti 22 mwaka huu na watacheza
mechi maalumu ya kirafiki Agosti 23 ndani ya dimba la kisasa la Taifa,
jijini Dar es salaam.
“Baada
ya mechi wataenda Arusha Agosti 25 kuangalia vivutio vya utalii na
watalala huko. Watalala tena Dar es salaam na kuondoka tarehe 26 ya
mwezi wa nane”.
“Kwahiyo
ni ziara ambayo ni ndefu kidogo, watu ni wengi, tulifikiri timu
ingekuja peke yake, kumbe kuna mashabiki wanaotoka Hispania
kuwashangilia hao magwiji, nafakiri Watanzania tukae mkao wa kula,”.
Alifafanua Ssebo.
Kuhusu viingilio vya mechi hiyo, Ssebo alisema watakuwa na kiwango cha chini kinachoweza kulipwa na watanzania wengi.
“Tunawahakikishia watanzania kuwa wataangalia mechi hii kwa kiwango cha chini kabisa.”
“Naweza
kuthubutu kusema kuwa kiwango cha chini kabisa kitakuwa shilingi elfu 5
ambacho tunaamini Watanzania wa kawaida wataipata kwasababu tumewaambia
mapema kwa mwezi mzima.” Ssebo alisema.
“
Lakini kikubwa zaidi, ni kuwahakikishia watanzania kuwa ziara hii
itafungua milango ya kujiuza na kuuza vivutio vyetu vya utalii”.
“
kwahiyo ni zaidi ya mpira na sisi tunaamini kabisa kuwa tutakuwa na
uwezo wa kuuza vitu vyetu, kwasababu wao watakuja na mashabiki, halafu
Real Madrid TV watakuja kurekodi ziara nzima timu ikiwa Tanzania”.
Alisema Ssebo.
Hii
ni ziara ya kwanza kabisa kwa klabu ya Real Madrid kufanya barani
Afrika, hivyo ni bahati kwa Tanzania kuwa nchi ya kwanza kutembelewa na
timu kubwa ya Real Madrid.
0 comments: