RC NA RAS NCHINI KUJENGEWA UWEZO NA KUHUISHA UHAI WA UTEKELEZAJI WA MAJUKUMU YAO.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ally Idd akifungua mafunzo ya
Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala Mikoa nchini leo jijini Dar es salaam.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Hawa Ghasia akimpongeza Mgeni Rasmi Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ally Idd na mara baada ya
kufungua mkutano wa mafunzo ya Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala Mikoa
nchini leo jijini Dar es salaam.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ally Idd akitete jambo na
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Hawa Ghasia wakati wa mkutano wa
mafunzo ya Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala Mikoa nchini leo jijini Dar
es salaam.

Baadhi ya washiriki wa mkutano wa mafunzo ya Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala Mikoa nchini leo jijini Dar es salaam.
(Picha zote na Eleuteri Mangi-Maelezo)
Eleuteri Mangi-MAELEZO
21/07/2014
Viongozi
wa Wakuu wa Mikoa nchini wameaswa kufahamiana kama viongozi ili
kubadilishana uzoefu wa kujenga mtandao wa mawasiliano na mahusiano kwa
ajili ya kupashana habari na kushauriana.
Kauli
hiyo imetolewa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ally
Idd wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya Wakuu wa Mikoa (RC) na Makatibu
Tawala Mikoa (RAS) nchini leo jijini Dar es salaam.
“Jengeni
mshikamano wa mahusiano katika utendaji kazi wenu mkiimarisha maelewano
miongoni mwenu mtarahisisha utendaji na kuepuka migogoro isiyo ya
lazima” alisema Balozi Seif.
Balozi
Seif aliendelea kusema, “Tumieni nafasi hii kufahamiana muweze kujenga
mtandao wa mahusiano, mawasiliano mkiimarisha mashirikiano ili kuleta
maendeleo katika maeneo yenu ya kazi kwa manufaa ya wananchi”.
Balozi
Seif alisema kuwa kila kazi inachangamoto zake, katika kutekeleza
majukumu yao vizuri na kubainisha kuwa viongozi hawa baadhi yao wamekuwa
na misuguano ya hapa na pale ambayo husababishwa na mawasiliano
yasiyoridhisha.
Balozi
Seif alisisitiza kuwa dawa ya misuguano hiyo itapatikana kupitia
mafunzo hayo ya siku tatu ambapo viongozi hao watakumbushwa mengi
waliyoyasahau, watapata mengi ya kujifunza, kujikumbusha na kujinoa ili
kuhuisha uhai wa utekelezaji wa majukumu yao ambao utaleta mshikamano na
umoja miogoni mwa watendaji hao.
Naye
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Hawa Ghasia alipokuwa akimkaribisha
Mgeni Rasmi alisema kuwa mafunzo hayo yataimarisha mahusiano na
mawasiliano ya viongozi hao katika kutekeleza majukumu yao ili yapate
tija iliyokusudiwa.
Waziri
Ghasia amewaasa viongozi hao kuwa wasipofanya kazi kama timu hawawezi
kupata tija katika maeneo yao ya kazi hasa katika kuwaletea maendeleo
wananchi wanaowaongoza na nchi kwa ujumla.
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa Wakuu wa Mikoa ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa
Mbeya Abbas Kandoro akimshukuru na kumhakikishia Mgeni Rasmi Balozi
Seif kuwa wanamatumaini makubwa kuimarisha mahusiano kati yao vilevile
na wanasiasa wote na kuahidi kuwa watatoa huduma bora zaidi.
Aidha,
mikoa ya Lindi, Mtwara na Ruvuma viongozi wao hawatashiriki mkutano huo
kwa kuwa kwa sasa wapo kwenye ratiba ya ziara ya Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete katika mikoa hiyo.
Wakuu
wa mikoa hiyo waunganishwa kupata mfunzo kama hayo na Wakuu wa Mikoa na
Makatibu Tawala wa mikoa ya Zanzibar ambayo itapangwa kufanyika hapo
baadaye ambapo Serkali ya Mapinduzi imeahidi kushirikiana na Tasisi ya
Uongozi kutoa mafunzo hayo.
Mafunzo
hayo yameandaliwa na Taasisi ya Uongozi kwa lengo la kuwawezesha
viongozi hao kufahamu kwa kina umuhimu wa mawasiliano bora baina ya
viongozi wa kisiasa na watendaji Wakuu wa ngazi ya Mkoa ili kuimarisha
utoaji bora wa huduma kwa wananchi.
0 comments: