Na Richard Mwaikenda
Katibu Mkuu wa Chama tawala cha Zimbabwe cha
ZANU PF, Didymus Mutasa ameviponda vyama vya
upinzani kwamba havina mizizi, vimeletwa Afrika na
Nchi za Magharibi kunyonya rasilimali, si kwa lengo
la kuwanuifasha waafrika.
Mutasa amewaasa Watanzania kuwa makini na vyama
vya upinzani akidai havina dira wala mwelekeo wa
kuwasaidia wananchi na uanzishwaji wake ni
ubabaishaji.
Pia, amesema wanaCCM wanapaswa kuhakikisha
wanakiendeleza Chama Cha Mapinduzi(CCM)
kinabakia madarakani kwa kuwa ni chama chenye
mtazamo wa kimaendeleo.
Akizungumza jana katika kikao cha makatibu wakuu
wa vyama vya ukombozi kusini mwa Afrika, Katibu
Mkuu wa Chama cha ZANU-PF, Mutasa alisema
vyama vya upinzani si vyama makini.
Alisema vyama hivyo, haviwezi kuwasaidia wananchi
hasa kutokana na uanzishwaji wake kuwa ni wa
ubabaishaji na havina mtazamano wa maendeleo.
“Afrika hakuna vyama vya upinzani na watanzania
wasikubali kabisa, kwa kuwa vyama hivyo havina
mwelekeo hasa kutokana na kutokuwa na mizizi
katika uanzishwaji wake tofauti na vyama
tawala,’’alisema.
Alisema vyama vya upinzani vingi vimeletwa na nchi
za magharibi ili kuja kunyonya na kupora rasilimali
zilizo ndani ya Afrika, hivyo wasikubali kuvipa nafasi.
Mutasa alisema watanzania wasikubali kuona CCM
inaondoka madarakani na kuja Chama kingine, kwa
kuwa vyama hivyo havitakuwa na uwezo wa
kuwaletea maendeleo.
Katibu Mkuu huyo, alisema siri kubwa ya ushindi wa
ZANU-PF katika uchaguzi mkuu wananchi hiyo,
uliofanyika hivi karibuni na Rais Robert Mugabe
kushinda umetokana na Wazimbabwe kutokubali
kuwapa wapinzani nchi na usimamizi wa sera ya
uwekezaji.
“Tuna hakika tunapendwa na wazanzibabwe, hasa
kutokana na serikali kuwa wa wazi na kuhakikisha
inasimamia rasilimali za nchi na hata kusikiliza vilio
vyao. Hivyo, ushindi wetu ni sauti ya
Wazimbabwe,’’alisema.
Alisema hata kelele zao hazitusaidia hasa kutokana
na kuhoji kuwa Rais Mugabe ni mtu mzee na ana
umri mkubwa, mbona wao wanasahau kuwa Malkia
Elizabeth ni mzee kuliko nchi ya Zimbabwe.
“Malkia ni Mzee kuliko Zimbabwe yenyewe na bado ni
malkia wa Uingereza. Hivyo Mugabe ni Rais wetu na
bado wazimbabwe wanampenda,’’alisema.
Akifungua mkutano huo, Katibu Mkuu wa CCM,
Abdurahman Kinana alisema mkutano huo ni
muhimu kwa kuwa unavikutanisha vyama vilivyoleta
ukombozi na watatumia mkutano kujadili mambo
mbalimbali.
Alisema kila chama kitakuwa na agenda yake, katika
mkutano huo, ambapo agenda kuu itakuwa ni vijana
kutokana na changamoto lukuki anazokutana nazo.
Mkutano huo wa siku moja, ulimalizika jana kwa
viongozi hao hao kufikia maazimio mbalimbali ikiwa
ni sehemu ya kuamsha serikali zao kuboresha
maisha ya wananchi.
Ends..
0 comments: