Latest Articles

MAKAMU WA PILI WA RAIS ZANZIBAR, MHE. ABDULLA AFUNGUA MKUTANO MKUU WA 17 WA IIA


Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Hemed Suleiman Abdulla (kulia) akipokea tuzo kutoka kwa Rais wa Taasisi ya Wakaguzi wa Ndani nchini Tanzania (IIA) CPA, Dkt. Zelia Njeza (wa pili kushoto) mara baada ya kufungua Mkutano Mkuu wa Mwaka wa 17 wa IIA. 


Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Hemed Suleiman Abdulla akifungua Mkutano Mkuu wa Mwaka wa 17 wa taasisi ya IIA, jijini Arusha. 

CPA Benjamin Mashauri Mkaguzi Mkuu wa ndani Tanzania Bara akizungumza kwenye mkutano huo.

Rais wa Taasisi ya Wakaguzi wa Ndani Tanzania (IIA), CPA Dkt. Zelia Njeza akizungumza na Wataalamu viongozi wa kada hiyo ya wakaguzi wa ndani katika mkutano Mkuu wa 17, wa mwaka, jijini Arusha.

Wakaguzi wa Ndani nchini Tanzania (IIA), na wadau wengine wakiwa katika mkutano huo.

Na Mwandishi Wetu, Arusha

MAKAMU wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Hemed Suleiman Abdulla amewataka Wakaguzi wa Ndani nchini Tanzania (IIA), kufanya kazi kuendena na mabadiliko ya kukua kwa teknolojia, ikiwa ni pamoja na kutumia changamoto za kiuchumi katika mataifa ya Afrika kama fursa kuweza kufikia malengo yao.

Akizungumza kwa niaba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, Makamu huyo wa Pili wa Rais, Mhe Suleiman Abdulla amesema ipo haja kwa wakaguzi wa ndani kuendana na mabadiliko ya ukuaji wa teknolojia ili kuongeza tija katika utekelezaji wa majukumu ya Wataalamu wa kada hiyo.

"Serikali itaendelea kushirikiana na wakaguzi wa ndani ili kuendelea kuimarisha shughuli za maendeleo ya wananchi na Taifa kupitia kazi za wakaguzi, kubwa zaidi ni kuendelea kuwa wabunifu, na uwajibikaji katika kazi hiyo.

Mhe. Makamu wa Pili wa Rais amebainisha kuwa kada ya ukaguzi wa ndani ni ya msingi katika kuongeza tija na chachu ya maendeleo kwenye taasisi za umma na binafsi kwani inaelekeza kuzingatiwa maadili na miiko ya kazi, hivyo kuondokana na dhana ya kukinzana na Serikali licha ya kuwa imekuwa msaada mkubwa kwa kile kuibua mambo mbalimbali yanayo kinzana na maendeleo ya taasisi na Taifa kwa ujumla.

Akizungumzia suala la urasimishaji, wa Sheria ya taaluma ya ukaguzi ambayo ndio miongoni mwa ajenda za msingi kwa IIA, Mhe. Suleiman Abdulla amesema tayari Serikali imeendelea na mchakato katika kupata Suluhu ya uwepo wa Sheria itakayo ongoza na kusimamia kada ya ukaguzi wa ndani kwa maendeleo endelevu.

Kwa upande wake Rais wa Taasisi ya Wakaguzi wa Ndani nchini Tanzania (IIA) CPA, Dkt. Zelia Njeza amesema kwa muda mrefu kada hiyo imekuwa ikikabiliwa na changamoto kadhaa ikiwemo kupatikana kwa Sheria ya wakaguzi wa ndani pamoja na muundo utakao saidia kufikisha ajenda na mawazo yatolewayo na kazi ya wakaguzi katika taasisi zao.

"Kiu yetu kubwa ni kuona Serikali inafanyia kazi ombi letu la kuwepo kwa Sheria ya ukaguzi wa ndani, na tunashukuru mchakato wa kufanikisha hilo umesha anza hivyo tunaomba kufanyiwa kazi kwa haraka na kukamilika ili tuweze kuendana na kasi ya mabadiliko tunayoyaongelea katika mkutano huu wa 17 wa mwaka. Pia tunaomba miundo ya wakaguzi wa Ndani pia iweze kuangaliwa maana asilimia kubwa bado hawako vizuri kwenye miundo yao," alisema CPA, Njeza Rais wa IIA nchini Tanzania.

Katika hatua nyengine, Dkt. Njeza akizungumzia suala la umuhimu wa maboresho ya muundo wa ripoti za kazi za wakaguzi kuzingatiwa katika taasisi mbalimbali kwa kuzingatia mnyororo wa Uongozi.

"Mkaguzi wa ndani anatakiwa kuripoti kwa Mkuu wa Taasisi, Utawala na wakati mwingine kwenye Bodi ya Uongozi moja kwa moja, hivyo tunaomba miundo hiyo pia iangaliwe ili kuongeza tija itokanayo na kazi ya ukaguzi wa ndani nchini." Alisema rais wa (IIA).

Naye Mkaguzi Mkuu wa ndani Tanzania Bara, CPA Benjamin Mashauri akizungumza katika mkutano huo, amesema zipo changamoto muhimu ambazo zikifanyiwa kazi kada hiyo itaendelea kuthaminika zaidi na mchango wake kuonekana wazi.

Miongoni mwa changamoto hizo ni pamoja na kuwepo kwa viongozi wa taasisi kujichukulia maamuzi pasi na kufata taratibu za kisheria suala ambalo lina ondoa hadhi ya kada hiyo katika mazingira ya utawala bora.

"Bado Kuna taasisi za umma na binafsi wakaguzi wa ndani, mfano wakati mwingine wakaguzi wanakosa vitendea kazi ikiwemo Kompyuta, magari, suala ambalo linadhohofisha ufanisi wakati wa utekelezaji wa majukumu ya mkaguzi wa ndani," alisema CPA Mashauri.

Katika mkutano huo Mkuu wa 17 wa mwaka kwa wakaguzi wa Ndani Tanzania (IIA), zaidi ya washiriki 70 kutoka mataifa mbalimbali barani Afrika yameshiriki, ukitanguliwa na jukwaa la viongozi wa taasisi, huku lengo kuu ikiwa ni kubadilishana uzoefu juu ya namna bora ya kufanya kazi za wakaguzi katika taasisi na kuleta tija kwa wananchi katika mataifa yao.
read more

VYAMA VYA USHIRIKA BADILIKENI

SERIKALI imeendelea kutoa msisitizo kwa Vyama vya Ushirika na kuvitaka kujenga misingi imara ya ushirika ili kumlinda mkulima badala ya kumnyonya na kumdhulumu haki zake.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe (Mb) tarehe 1 Oktoba 2024 wakati akizindua Kiwanda cha Kubangua Korosho cha TANECU kilichopo Newala, Mkoani Mtwara.

Waziri Bashe amesema safari ya kuvikwamua vyama vya ushirika haikuwa rahisi kwa kuwa vilikuwa na madeni ya zaidi ya shilingi bilioni 17 na benki zilikuwa zinawakwepa kuwakopesha. “Kujenga ushirika imara ndiyo msingi wa kumsaidia mkulima mdogo. Leo tasnia ya korosho ina taswira tofauti na sasa tunajadili kiwanda cha TANECU cha kubangua korosho,” amesema Waziri Bashe.

Aidha, Waziri Bashe amekipongeza Chama Kikuu cha Ushirika cha TANECU Ltd. kwa kuwa mfano mzuri wa kuonesha ushirika unaozidi kuwa imara kwa kuhakikisha uwekezaji huo wa kiwanda ni wa wakulima wenyewe. “Naelekeza pia kijengwe kiwanda kingine kama hiki kule Tandahimba ili kiwe tayari wakati wa msimu wa mwaka ujao,” amesema Waziri Bashe.

Kiwanda cha TANECU kimegharimu shilingi bilioni 3.4 na kina uwezo wa kubangua tani 3,500 kwa mwaka. Mkakati ni kuwa na viwanda 20 vya Kubangua Korosho chini ya TANECU katika Mkoa wa Mtwara ambapo 10 vitajengwa Newala (tayari 1 kimezinduliwa); na 10 vitajengwa Tandahimba.









read more

WANANCHI MNAFANYA KAZI ZENU KWENYE MTANDAO MPO SALAMA SERIKALI IMETUNGA SHERIA KULINDA DATA ZA MTU BINAFSI

 


Na. Vero Ignatus Arusha

Waziri wa Habari ,Mawasiliano Teknolojia ya habari Jerry Slaa, amefungua kongamano wa siku mbili (Connect2Connect Summit)ambapo umewakutanisha wadau wote wa Mawasiliano nchini pamoja na wadau wengine ambapo amesema Watanzania zaidi ya Mil.75 wana simu za mkononi 35% wanamtandao wa intaneti ambapo mwaka mei 2023 Serikali ilizindua mkakati wa ujenzi wa minara 758 kupitia USAF mfuko uliotengenezwa na serikali ambapo kila mtoa huduma anachangia ili kupeleke huduma

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa kongamano hilo Mhe. Always alisema minara mingine 636 mradi huo utaanza Oktoba 2024 huku akiwataka wananchi wanaofanya shughuli zao kupitia mitandao wapo salama zaidi na Serikali imetunga Sheria ya kulinda data za mtu binafsi katika matumizi ya mtandao na kila mtumiaji analindwa na hairuhusiwi kutumia data za mtu bila ridhaa yake.

Aidha Waziri Slaa,amesema hadi sasa 89% ya Watanzania wanapata huduma mtandao lengo likiwa Wananchi wote wapate huduma ya mtandao wa Internet,simu ,habari ,redio na televisioni yakuwemo maeneo ya Utalii ambayo yamepewa kipaumbele

Joseph Muhere, ni Mkurugenzi wa biashara Kampuni ya smu za mkononi,Airtel , amesema mwaka 2013 kampuni hiyo ilifunga mtambo mpya Submarinecable ambao ni mkubwa wenye uwezo wa kupokea na kutumia data kwa kiwango kikubwa ,uwekezaji huo umefanywa kwa ajili ya Watanzania na nchi jirani kwajili ya mawasiliano.

"Airtel mwaka huu 2024 inaendelea kufangua huduma zake za mawasiliano katika miji na Vijiji ambapo kwa mjini kuwezesha kupata huduma ya 3G,4G,5G na Kampuni inaendelea na Uwekezaji na upanuzi wa mtandao maeneo ya Vijiji ili kuwezesha kupata huduma ya 3G 4G na 5G"Amesema .

Muhere,alifafanua kuwa lengo la Mkutano huo wa 8 ni kuwaleta Wadau wote pamoja katika teknolojia, ambapo kampuni hiyo inaendelea kuvifikia Vijiji vyote ambavyo havijafikiwa na huduma hiyo ambapo sasa wanajenga huduma ya 5G kwa ajili ya wateja Ujenzi ambao unaenda sambamba na kuhakikisha gharama zinakuwa nafuu.

Kwa upande wake injinia Cecil Mkomola Francis mkurugenzi wa ufundi na Uendeshaji wa Shirika la mawasiliano Tanzania TTCL amesema wanadhamana kubwa ya kutoa huduma ya mawasiliano, kupitia mkongo wa mawasiliano wa Taifa kwani wameendelea kufanya kazi na kuhakikisha kuwa nchi inaongea kwa kuunganishwa mikoa wilaya ambapo jumla ya wilaya 106 zimeunganishwa Tanzanzania bara Kati ya wilaya 139,mkongo huo ndio kiungo kikuu cha Mawasiliano na Intaneti.

Amesema kuwa kazi kubwa waliyonayo kama Shirika ni kutoa mchango mkubwa wa mawasiliano kuhakikisha kwamba wanafikisha huduma kwa Wananchi na kupungiza gharama za matumizi.

Kwa upande wake ,Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Shirika la mhandis Francis Mkomola,amesema Shirika hilo lina dhamana kubwa ya kutoa huduma bora za mawasiliano kupitia mkongo wa taifa ambao ulianza kutekeleza mwaka 2013.

Vilevile wameunda mkongo huo na nchi jirani za Kenya,Uganda ,Rwanda,Burundi ,Zambia,Malawi na kuna maunganusho yanayoenda kwenye mpaka na Msumbijina sasa wanaanza kushughulikia maunganusho na nchi ya DRC Congo,kupitia ziwa Tanganyika hadi mji wa Kalemii Nchini DRC pia wanashugulikia maunganisho kwenda kwenye kituo kilichopo baharini hadi Mombasa Nchini Kenya.

TTCL inaendelea kutoa mchango wa mawasiliano kuhakikisha mkongo unaojengwa inakuwa na ubora wa hali ya juu kwa lengo la kufikisha huduma kwa Wananchi na kupunguza gharama ambapo Tanzania ni kiunganishi kikuu cha Mawasiliano kwenye ukanda wa nchi za EAC na SADC, wilaya ambazo hazijaunganishwa kwenye mkongo wa taifa zitaunganishwa mwaka huu na wakandarasi wapo wanaendelea na shughuli hiyo

Mkutano huu umehusisha wadau wote wa mawasiliano nchini Tanzania, Somalianchi za Afrika Mashariki na kusini kwa Afrika chini ya kauli mbiu ya ‘Meaningful Connectivity’.

Waziri wa Habari ,Teknolojia ya Mawasiliano ya habari Mhe.Jerry Slaa, amefungua kongamano wa siku mbili katika Hotel ya Gran Melia Jijini Arusha leo septemba 18,2024
Mhandisi Cecil Mkomola Francis mkurugenzi wa ufundi na Uendeshaji wa Shirika la mawasiliano Tanzania TTCL


Joseph Muhere, ni Mkurugenzi wa biashara Kampuni ya simu za mkononi,Airtel


Katibu Mkuu Wizara ya Habari ,Mawasiliano Teknolojia ya habari Mohamed Khamis Abdulla



Washiriki
read more

DC MPOGOLO ATAKA VIONGOZI KUWA NA MAHUSIANO MEMA

 Mkuu wa wilaya ya ilala Edward Mpogolo amewataka viongozi wa chama na serikali kuwa na mahusiano mazuri katika kazi zao.

Akiongea na viongozi wa chama na serikali katika ziara yake kwenye kata ya liwiti, tabata na kimanga Mpogolo ameeleza mahusiano ya viongozi hao yanasaidia kuelewa kazi zinazofanywa katika miradi ya maendeleo hivyo wasione ugeni kushirikiana.

Ameongeza kuwa hata katiba ya nchi inatambua mahusiano na mfumo wa chama chenye dhamana  na serikali iliyopo madarani kupitia ilani inayotekelezeka. 

Akielezea kuhusu maandalizi ya uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka huu amewataka wananchi kushiriki, kujiandikisha na kupiga kura na kudumisha umoja, upendo na mshikamano.

 Amesema viongozi wahamasishe wananchi kujiandikisha katika daftari litalikuwa katika maeneo ya mitaa wanayoishi zoezi ambalo litaanza tarehe 11 hadi 20 mwezi ujao na uchaguzi ni novemba 27 mwaka huu. 

Akijibu kero zilizowasilishwa katika mkutano uwo Mpogolo amesema kero zinazohusu elimu hasa uzio katika shule ya sekondari liwiti iliyopakana na shule mbili za msingi halmashauri itahakikisha inatatuliwa kwa wakati. 

Kero nyingine aliyoitolea ufafanuzi ni kuhusu mto msimbazi ambao ni kilio kwa wananchi na serikali tayari imeona na kuanza kutafuta njia ya kuondoa kero hiyo kwa kuwa mto uwo umekuwa na tabia ya kuhama hama. 

Kuhusu kero ya barabara katika kata ya tabata, liwiti na kimanga ameleeza barabara hizo zipo zilizoingia katika mradi wa Dmpd na nyingine zitashughulikiwa na tarura.

Aidha Mkuu wa wilaya ya ilala Edward Mpogolo amewataka viongozi, wazazi na walezi kusimamia maadili ya watoto kwa ujumla hasa waliomaliza darasa la saba wasipate mimba na magonjwa ya zinaa.









read more

DKT. BITEKO AHIMIZA WANAWAKE KUTUMIA MIFUKO YA UWEZESHAJI WANANCHI KIUCHUMI

 Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati


Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amewahimiza wanawake nchini kutumia fursa ya mifuko ya uwezeshaji wananchi kiuchumi kwa ajili ya kukopa na kujiongezea vipato.

Dkt. Biteko ametoa rai hiyo leo Septemba 14, 2024 mkoani Singida wakati akimwalilisha Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa kwenye Kilele cha Maonesho ya Saba ya Mifuko na Programu za Uwezeshaji kwa Mwaka 2024.

“ Wanawake tumieni fursa iliyoweka na Serikali ya Mifuko ya Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi ili muweze kukopa na kupata manufaa kutokana na mikopo hiyo. Natoa wito kwa benki zote nchini muwaaamini wanawake kwenye mikopo hii, mahali popote ukiona mwanamke anashughulika ujue faida inayopatika ni kwa familia yote,” amesema Dkt. Biteko.

Dkt. Biteko amebainisha kuwa Mhe. Rais Dkt. Samia alitoa wito kwa benki kuongeza kiwango cha kutoa mikopo kwa wananchi huku akitolea mfano Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB) ambayo mwaka 2020 ilitoa shilingi bilioni 63 na hadi kufikia Agosti 2024 imetoa mikopo kiasi cha shilingi bilioni 337.

Ametaja takwimu za utoaji mikopo hiyo kutoka Benki ya TADB kuwa wanaume ni asilimia 58.1, vijana asilimia 19 na wanawake asilimia 22.4 huku akisisitiza benki nchini kuendelea kuongeza kiwango cha utoaji mikopo kwa wanawake.

“Mabenki endeleeni kuwaamini Watanzania, wakopesheni, punguzeni masharti lakini wenye uwezo wa kulipa wapeni mikopo ili waweze kufanyakazi.” Amesisitiza Dkt. Biteko.

Sambamba na hayo Dkt. Biteko amezindua Mwongozo wa Uratibu na Usimamizi wa Mifuko na Programu za Uwezeshaji ili iwe nyenzo ya kuimarisha utendaji wa mifuko na programu za uwezeshaji kwa lengo la kuondoa changamoto zilizopo hasa mikopo chechefu ili kufikia malengo yaliyokusudiwa katika kukuza uchumi na kupunguza umaskini katika jamii.

Akizungumzia Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Tanzania Bara utakaofanyika tarehe 27 Novemba 2024. Amewaasa wananchi wa Singida na Watanzania kuchagua viongozi kwa kuzingatia sifa zao na si dini, fedha wala ukabila.

“ Ushiriki wenu katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa utawezesha kupata Viongozi wa Serikali za Mitaa ambao watachochea shughuli za uchumi na kusimamia vyema miradi pamoja na mifuko na programu za uwezeshaji zitakazokuwa zinaletwa katika maeneo yenu.” Amesema Dkt. Biteko.

Kwa upande wake, Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba amesema kuwa Programu ya Uwezeshaji na elimu iliyotolewa mkoani Singida imegusa akina mama wengi na uwezeshaji huo utabadilisha maisha ya wananchi wa mkoa huo.

“ Programu za skimu za umwagiliaji zinalenga kupunguza umaskini kwa mtu mmoja mmoja na uwezeshaji wananchi kiuchumi umeleta mabadiliko makubwa mkoani kwetu,” amesema Dkt. Nchemba.

Katibu Mtendaji wa Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, Bi. Ben’g Issa amesema kuwa Serikali imekuwa ikifanya jitihada mbalimbali za kuwawezesha wananchi kiuchumi kwa kuwa na sera za kuwezesha wafanyabiashara wadogo.

Ambapo imeanzisha mifuko na programu za uwezeshaji wananchi kiuchumi na kutoa ruzuku katika sekta mbalimbali kwa kuwa bado wafanyabiashara wadogo hawapati mikopo kwa urahisi.

“ Serikali imekuwa ikifanya maonesho ya mifuko na programu za uwezeshaji ili kujenga uelewa kwa wananchi na kuonesha mifuko hii inavyoweza kubadilisha maisha yao, pia imeendelea na vituo vya uwezeshaji wananchi kiuchumi katika mikoa yote Tanzania Bara ili kuhakikisha huduma mbalimbali ikiwemo mikopo, uongezaji thamani mazao, elimu ya kodi inawafikia wananchi.” Amesema Bi. Issa.

Aidha amemshukuru Rais Samia kwa kutoa fedha kwa ajili ya kuimarisha programu ya Imarisha Uchumi na Mama Samia nchini inayolenga kuhakikisha wananchi wote wanapata fursa za kushiriki katika shughuli za uchumi na kukuza vipato vyao.

Maonesho ya Mifuko na Programu za Uwezeshaji hayo yameongozwa kwa kaulimbiu inayosema “Shiriki katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Unufaike na Fursa za Uwezeshaji".
read more

WAVISHWA NISHANI

    Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Wananchi wa Tanzania Jenerali Jacob John Mkunda kwa niaba ya Mhe Rais na Amiri Jeshi Mkuu Dkt Samia Suluhu Hassan amewavisha nishani mbalimbali Majenerali, Maafisa na Askari wa JWTZ mjini Morogoro tarehe 14 Septemba 2024.

Nishani hizo ni Nishani ya Utumishi Uliotukuka, Nishani ya Utumishi Mrefu, Nishani ya Utumishi Mrefu na Tabia Njema, Nishani ya Miaka 60 ya Muungano pamoja na Nishani ya Miaka 60 ya JWTZ.






read more

WAZIRI WA AFYA JENISTA MHAGAMA AFANYA ZIARA LEO TAASISI YA MOYO (JKCI)

 

Mkurugenzi wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete akimkaribisha Mhe. Waziri wa Afya . Jenista Mhagama mara alipowasili katika Taasisihiyo wakati wa ziara yake iliyofanyika leo 11, Septemba 2024.

  Mkuu wa Kitengo cha TEHAMA na TAKWIMU Taasisi ya Moyo JKCI. Lazaro Swai (wa pili kulia) akimpatia maelezo Mhe. Jenista Mhagama juu ya mfumo wa Kiongozi foleni ambao upande mmoja una lengo la kuongoza foleni ya watu wanaokuja kusalimia wagonjwa wao upande wa pili ni kuongoza foleni ya wagonjwa wanaokuja kupatiwa matibabu 
  Mhe. Waziri wa Afya Jenista Mhagama akimsikiliza Mtoto Ally Mwandu aliefanyiwa upasuaji Taasisi ya moyo ya Jakaya Kikwete wakati akikabidhiwa UA mara alipofanya ziara katika Taasisi hiyo leo 11,Septemba 2024.
Mhe. Waziri wa Afya Jenista Mhagama  akizungumza na baadhi ya ndugu wa wagonjwa mara alipofanya ziara ya kutembelea Taasisi ya moyo ya Jakaya Kikwete leo Septemba 11, 2024 

Mhe. Waziri wa Afya Jenista Mhagama akisaini kitabu cha wageni mara alipofanya ziara ya kuitembelea Taasisi ya moyo ya Jakaya Kikwete leo Septemba 11, 2024 Jijini Dar es Salaam. 
Mkurugenzi Mtendaji akimkabidhi zawadi Mhe. Waziri wa Afya Jenista Mhagama leo wakati alipofanya ziara katika Taasisi ya moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI)

  Mhe. Waziri wa Afya Jenista Mhagama akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Taasisi ya moyo ya Jakaya Kikwete leo Jijini Dar es Salaam.
read more