MKURUGENZI TET AWATAKA WADAU WA ELIMU KUTEMBELEA BANDA LAO SABASABA

 Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania(TET) Dkt. Aneth Komba ametoa rai kwa wadau mbalimbali wa elimu nchini kutembelea katika maonesho ya kibiashara ya kimataifa ya Dar es salaam hususani kufika banda la TET ili kuweza kufahamu utekelezaji wa Mtaala ulioboreshwa.


Ameyasema hayo leo Julai 9, 2024 wakati aliopotembelea  maonesho hayo yanayoendelea viwanja vya sabasaba jijini Dar ea Salaam ambapo ameeleza kuwa TET imeendelea kutoa elimu kwa wadau nchini kwa kuwaelewesha maboresho ya Mitaala yaliyofanyika, ambayo utekelezaji wake ulianza mwezi Januari 2024.

"Wadau tembeleeni katika banda letu hapa mtapata kufahamu masuala mengi kuhusiana na utekelezaji wa Mitaala iliyoboreshwa." amesema Dkt.Komba.

Pia, amesema kuwa TET inaendelea na uuzaji wa vitabu vya kiada kwenye maonesho hayo, hivyo kuwakaribisha wananchi wanaohitaji vitabu vya kiada vya Mitaala yote.

Katika ziara hiyo, Dkt.Komba alipata pia nafasi ya kutembelea katika mabanda mengine yakiwemo NECTA, NACTVET NA TBC.

0 comments: