ASHUSHIWA KIPIGO BAADA YA KUMWAGA PILIPILI YA MUUZA PWEZA JIJINI DAR ES SALAAM KARIAKOO.

  Msaidizi wa Dereva (Kondakta), mwenye Gari lenye namba za Usajili T974 DMP  amejikuta akishushiwa kipigo cha mbwa mwitu baada ya kumwaga pilipili ya mfanya Biashara wa Pweza mara alipokuwa akiisogeza Pikipiki iliyokuwa njiani na kujikuta anamwaga pilipili ya mfanya Biasha huyo Mitaa ya K/Koo leo Tarehe 10/6/2024 na kuitiwa mwizi na kukimbilia katika Gari hilo hapo ndipo Wananchi wenye hasira  walimkimbiza na kumshusha na kumpa kipigo nakujikuta nguo ya kifuani hana na akidai kupoteza hesabu aliyokuwa nayo japo haikufahamika mara moja ni kiasi gani cha pesa. (PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA)


Kondakta akipata kipigo kutika kwa Wananchi eneo la Kariakoo

0 comments: