TANZANIA YA KWANZA AFRIKA KUTUMIA MASHINE YA KUFUATILIA WAGONJWA NYUMBANI

    Mkuu wa Mkoa wa  Dar es Salaam Mhe. Albert Chalamila mashine ya Dozee iliyotengenezwa na Sakaar Health Tech LTD ambayo inatumika kuwafuatilia wagonjwa  wa moyo wakiwa nyumbani ili kujua hali zao na kutoa msaada wa haraka endapo utahitajika.


***********************************************************************************************************************************************************************************


Kwa mara ya kwanza barani Afrika Taasisi ya moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na Sakaar Health Tech LTD wamezindua rasmi mashine  maalum  itakayotumika  kufuatilia wagonjwa  wa moyo wakiwa nyumbani ili kujua hali zao na kutoa msaada wa haraka endapo utahitajika.


Kufuatia uzindunzi wa mashine hiyo iitwayo Dozee Tanzania sasa imekuwa nchi ya tatu Duniani kutoa huduma hivyo huku ikiwa nchi ya kwanza barani Afrika.


 Akizungumza wakati wa uzinduzi huo jana jijini Dar es Salaam,mkuu wa mkoa huo Mhe. Albert Chalamila alisema teknolojia hiyo inapunguza gharama za matibabu na endapo kutawakuwa na wahuduma wachache  ni rafiki pia.


 Kazi kubwa ni kutumia na kuwekeza ili tuweze kupata kwenye ukubwa wake zaidi  na huduma hii itamuwezesha mgonjwa kufuatiliwa na wataalamu wetu akiwa nyumbani kwa umakini na ukarimu ule ule nawashukuru wadau ambao wameshirikiana na serikali ikiwa sehemu ya sera ya kurudisha kwa jamii”, alisema Mhe. Chalamila.


 Aidha ametoa rai kwa wananchi kuhakikisha wanafuata ushauri wa wataalamu hasa wa kujikinga na magonjwa yasiyoambukiza ambapo  siku chache Waziri mkuu alitoa maelekezao ya  barabara ya Tanzanite kufungwa kwa siku ya jumamosi asubuhi  ili watu wafanye  mazoezi.


Mhe. Chalamila alisema  Mhe. Rais  Dkt. Samia Suluhu Hassan  amewekeza kwa kiasi kikubwa katika afya ya watanzania ili kuhakikisha kuwa na watu ambao wana afya bora  na kuweza kuwa na mchango wa kuleta maendeleo.


“Serikali imefanya mambo mengi ukiende kwenye uzazi amepunguza vifo lakini amejengea uwezo Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (KCI) na magonjwa ya moyo yapo kazi iliyopo ni kuhakikisha tunakabiliana nayo kwa kuwekeza kwenye teknoloji.


Pia ameipongeza Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)  kwa kumuunga mkono Mhe. Rais Samia ikiwa na ubunifu huo wa kuendelea kutoa huduma kwa wananchi .


Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Peter Kisenge  alisema ili kwenda na teknoloji na kuwahudumia wananchi wamekuja na njia mbadala ya kisasa ya kuhudumia wagonjwa nyumbani mara watakapofanyiwa upasuaji au kufanyiwa tiba hapo JKCI kama upasuaji mdogo wa moyo ka kutumia mtambo wa  Cathlab.


“Sasa kwa hawa wagonjwa mara nyingine wanabadilika mapigo ya moyo yanakwenda kasi sana kwahiyo tunachofanya hii Dozee inawekwa chini ya kitanda na unaweza kugundua mapigo yao ya moyo na presha na jinsi wanavyopumua  na kama kukitokea tatizo unaweza kugundua.


Aliongeza, “Hivi juzi kuna mgonjwa alitibiwa kwetu tukamwekea Dozee usiku mapigo ya moyo yakapanda hadi 140 na wakati mwingine 160 tukapata alarm tukampigia simu na tukarudisha na sasa anaendelea na matibabu”, alisema Dkt. Kisenge.


Dkt. Kisenge ambaye pia ni daktari bingwa wa moyo alisema  teknolojia hiyo itasaidia  kuwahudumia wagonjwa vilevile itapunguzia gharama kwa ambao walikuwa walazwe hospitalini kwa wiki mbili sasa wanakaa siku tano na baade kufuatiliwa wakiwa nyumbani.

0 comments: