BODI YA WADHAMINI YAFANYA KIKAO LEO DAR ES SALAAM

  Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Asha Izina ambaye pia ni Mratibu wa huduma za Afya ya Uzazi na Mtoto  Mkoa wa Rukwa akiongoza kikao cha nne cha Bodi hiyo kilichofanyika leo jijini Dar es Salaam.

  Katibu wa Bodi ya Wadhamini ya Taasisi ya Moyo Jakaya  Kikwete (JKCI) ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Dkt. Peter Kisenge akitoa taarifa ya utendaji wa kazi zilizofanywa na taasisi hiyo kwa kipindi cha miezi mitatu ya Aprili hadi Juni 2023 katika mwaka wa fedha wa 2022/23 wakati wa kikao cha nne cha Bodi hiyo kilichofanyika leo jijini Dar es Salaam.
  Mkurugenzi wa Tiba Shirikishi wa Taasisi ya Moyo Jakaya  Kikwete (JKCI) Dkt. Delilah Kimambo akiwaeleza wajumbe wa Bodi ya Wadhamini ya Taasisi hiyo upatikanaji wa damu kwa wagonjwa wanaofanyiwa upasuaji wa moyo wakati wa kikao cha nne cha Bodi hiyo kilichofanyika leo  jijini Dar es Salaam.
  Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini ya Taasisi ya Moyo Jakaya  Kikwete (JKCI) ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Prof. Mohamed Janabi akichangia mada wakati wa kikao cha nne cha Bodi hiyo kilichofanyika leo  jijini Dar es Salaam.
  Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini ya Taasisi ya Moyo Jakaya  Kikwete (JKCI) ambaye pia ni Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) Prof. Appolinary Kamuhabwa akichangia mada wakati wa kikao cha nne cha Bodi hiyo kilichofanyika leo jijini Dar es Salaam.

Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini ya Taasisi ya Moyo Jakaya  Kikwete (JKCI) Mhe. Balozi Mwanaidi Sinare akichangia mada wakati wa kikao cha nne cha Bodi hiyo kilichofanyika leo  jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya Viongozi wa Menejimenti ya Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakimsikiliza Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Taasisi hiyo Asha Izina wakati wa kikao cha nne cha bodi hiyo kilichofanyika leo  jijini Dar es Salaam.
 

0 comments: