Na Mwandishi wetu
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Mohamed Mchengerwa amesema kuwa michoro kwa ajili ya ujenzi wa Uwanja wa Mpira wa Miguu jijini Dodoma umekamilika na mkandarasi atakabidhiwa eneo Machi 2023.

Waziri Mchengerwa ameishukuru Wizara ya Fedha kwa kutoa fedha za kuanzia katika ujenzi wa viwanja hivyo ambapo amesema tayari zabuni kwa ajili ya ujenzi wa eneo changamani la Michezo jijini Dar es Salaam imeshatangazwa.
Vilevile, Mhe.Mchengerwa ameeleza kuwa Wizara hiyo inaendelea kufanya mageuzi makubwa ambapo imeanzisha Kampeni ya Sanaa mtaa kwa mtaa yenye lengo la kuibua vipaji kuanzia ngazi ya chini, huku akiwapongeza wasanii kwa kutumia vipaji vyao kuitangaza Tanzania.
Aidha, Mhe. Mchengerwa amesema Wizara imeendelea kufanya mapinduzi katika Sekta zake ikiwemo mchakato wa kupata Vazi la Taifa, Mdundo wa Taifa pamoja na kutoa mikopo kwa Wasanii.
Katika Hatua nyingine, Mhe. Mchengerwa ameeleza kuwa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limeitangaza Tanzania kuwa namba Tano katika nchi zenye ligi bora Afrika na namba 39 katika viwango vya kimataifa.

0 comments: