UBALOZI WA KUWAIT NCHINI WAJUMUIKA KATIKA FUTARI


 Balozi wa Kuwait nchini Tanzania Mhe Jasem Al-Najem (wa tata kulia) na Dr. Waliyd Shuaib Msaidizi Katibu Mkuu wa maswala ya Quran Tukufu na Masomo ya Kiislamu  kutoka Wizara ya Wakfu na Maswala ya Kiislamu nchini Kuwait wajumuika na waislamu na wakazi wa moja ya msikiti Dar es salam katika futari iliyotaarishwa na Ubalozi ikiwa ni mwendelezo wa mpango wa kufuturisha kutoka Chombo cha Baytul Zakat, Wakfu na Mali ya Amana cha Kuwait.

Futari hiyo ilihudhuriwa na Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Mhe. Majid Mwanga, wafanyabiashara, na wakaazi wa eneo hilo wakiwemo wanawake na watoto. Mkuu wa Wilaya  alitoa shukrani kwa wasamaria wema wa Kuwait akitarajia futari kama hiyo iendelee katika maeneo mengine nchini.

0 comments: