WAGONJWA 64 KUFANYIWA UPASUAJI TAASISI YA MOYO JAKAYA KIKWETE (JKCI)
Posted by khamisimussa77@gmail.com at 4:42 PM
Daktari
Bingwa wa upasuaji wa Moyo na Mishipa ya damu kutoka Hospitali ya B.L.K
ya nchini India, Ajal Kajul (kulia) akizungumza na waandishi wa habari kuhusu
uhusiano wao na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) ambapo kwa pamoja
wameweza kuwafanyia upasuaji bila kufungua kifua
wagonjwa 64. Kushoto ni Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo Peter
Kisenge.
Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya
Kikwete (JKCI), Peter Kisenge (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari kuhusu
uhusiano wao na Hospitali ya B.L.K ya nchini India ambapo kwa pamoja
wameweza kuwafanyia upasuaji wa kufungua bila kufungua kifua
wagonjwa 64. Kulia ni Daktari Bingwa wa upasuaji wa Moyo na Mishipa ya
damu kutoka Hospitali ya B.L.K ya nchini India, Ajal Kajul.
Wafanyakazi
wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakimsikilliza Daktari Bingwa
wa upasuaji wa Moyo na Mishipa ya damu kutoka Hospitali ya B.L.K ya
nchini India (hayupo pichani) wakati akizungumza na waandishi wa habari
kuhusu uhusiano wao na Taasisi hiyo ambapo kwa pamoja wameweza
kuwafanyia upasuaji wa kufungua na kufungua kifua wagonjwa 64. (Picha
na JKCI)
MADAKTARI
kutoka Taasisi ya Moyo ya Jakaya kikwete kwa ushirikiana na wenzao wa
Hospitali ya B.L.K ya nchini India wamewafanyia wagonjwa 64 upasuaji wa
moyo ambao ni wa kufungua na bila kufungua kifua.
Kati
ya hao wagonjwa nane walifanyiwa upasuaji wa kufungua kifua na 52
walifanyiwa upasuaji wa bila kufungua kifua (catheterization) kwa
kutumia mtambo wa Cathlab.
Pia
madaktari hao wamepata mafunzo ya kufanya upasuaji wa milango miwili ya
moyo ambapo awali huduma hiyo ilikuwa haitolewi kwenye taasisi hiyo .
Mafunzo
hayo ya siku tano yaliyo ongozwa na wataalamu kutoka Hosipitali ya BLK
ya Nchini India itasaidia serikali kuokoa zaidi ya milioni 30 ambazo
zingetumika kwaajili ya matibabu ya mgonjwa wa moyo wenye uhitaji wa
upasuaji wa milango miwili ambapo asilimia 25 ya wagonjwa wana uhitaji
huo.
Akizungumza
na Waandishi wa habari jana Dar es Salaam Daktari bingwa wa magonjwa ya
moyo Peter kisenge alisema kupitia kambi ya siku tano ya madaktari
nane wanaotibu maradhi ya moyo ,Wataalamu wa usingizi ,Wataalamu wa
kutoa damu kwenye mapafu ,kutoka Hosipitali ya BLK ya nchini India
imesaidia kutoa mafunzo ya uwekaji na upasuaji wa milango miwili kwenye
moyo kwa wagonjwa wenye matatizo hayo ambapo huduma hiyo itakuwa ya
kwanza kutolewa hapa nchini.
Mbali
na huduma hiyo Dk Kisenge alisema tayari madaktari watatu wa taasisi
hiyo wanaweza kutoa huduma ya uwekaji wa milango miwili ya damu kwenye
moyo huku Daktari mmoja akipata mafunzo ya miaka miwili nchini india.
Kuanza
kwa huduma hiyo alisema watasaidia watoto wadogo ambao milango yao
imeziba ambapo awali walikuwa hawafanyiwi upasuaji kutokana kutokuwepo
kwa ujuzi wa upasuaji wa milango hiyo.
Alisema
kwa wagonjwa 64 waliofanyiwa upasuaji katika taasisi hiyo
wangesafirishwa nchini india serikali ingepoteza zaidi ya bilioni 6 .
Kwa
upande wake Daktari Bingwa Upasuaji wa moyo na mishipa ya damu kutoka
Hosipitali ya BLK ya Nchini India Dk Ajal Kajul alisema wataendelea
kutoa ushirikiano kwa madaktari hapa nchini ambapo baadhi ya madaktari
walioambatana nao watabaki katika taasisi hiyo kwaajili ya kuendelea
kutoa mafunzo zaidi.
Dk.
Kaul alisema wataendelea kuonyesha ushirikiano wa kutoa ujuzi kwa
madaktari wa hapa nchini ambapo octoba mwaka huu watatoa mafunzo ya
upandikizaji wa figo,na wagonjwa wenye matatizo ya mgongo katika
Hosipitali ya Taifa ya Muhimbili.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)



0 comments: