HATIMAYE KINGA YA MASHAMBULIZI YA HIV YAPATIKANA

Wanasayansi nchini Marekani wamefanikiwa kutengeneza chembe chembe za kinga ya mwili zinazoweza kushambulia asilimia 99% ya HIV (virusi vinavyosababisha ukimwi) na hivyo kuzuia maambukizi kuendelea.
Utafiti huo uliofanywa kwa ushirikiano wa Taasisi ya Taifa ya Afya ya nchini Marekani na Kampuni ya madawa ya Sanofi, unaonesha chembe chembe hiyo ya kinga imetengenezwa kwa ajili ya kushambulia sehemu tatu muhimu za virusi na hivyo kuvifanya virusi hivyo kushindwa kuhimili mashambulizi yake.
Wataalam wa masuala ya UKIMWI wamesema kitendo hicho ni mafanikio yenye furaha, huku majaribio ya binadamu yakitarajiwa kufanyika mwakani, baada ya kukamilisha utafiti kwa nyani 24 na kuonyesha mafanikio makubwa.
Mwanasayansi mkuu wa SANOFI Dkt. Garry Nabe, amesema kinga hiyo ina nguvu zaidi kuliko kinga yoyote ya asili iliyowahi kutokea na yenye kiwango kikubwa cha ulinzi.

0 comments: