TUTASHIRIKIANA NA MAKAMPUNI BINAFSI KUPANGA MAKAZI YA WANANCHI- MEYA WA UBUNGO
Posted by khamisimussa77@gmail.com at 9:41 AM
Mstahiki
meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo, Jacob Masawe akizungumza na
wananchi wa Mtaa wa Kunguer kata ya Goba wakati wa Mkutano wa Upangaji
na Upimaji wa eneo hilo unaoendeshwa na Kampuni ya HUSEA, kulia ni Mwenyekiti wa HUSEA, Renny Chiwa na kushoto ni Mkurugenzi wa Mipango Miji na Vijiji, Prof John Lupala
Mwenyekiti wa HUSEA, Renny Chiwa akizungumza
na wananchi wa Mtaa wa Kunguer kata ya Goba wakati wa Mkutano wa
Upangaji na Upimaji wa eneo hilo na kuelezea namna kampuni yake
ilivyojikita katika kuhakikisha wanasaidiana na serikali kwenye utatuzi
wa migogoro na upangaji wa maeneo. Akiwa amekaa meza moja na Diwani wa
kata ya Goba Ibrahim Kenya (wa kwamza kushoto), Mkurugenzi wa Mipango Miji na Vijiji, Prof John Lupala.
Wananchi wakiwa wanaelezewa namna Mtaa wa Kunguru ulivyopimwa na kutakiwa kupangwa.
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
MSTAHIKI
meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo, Jacob Masawe amesema kuwa
eneo litalakolokuwa limepimwa na kugundulika ni eneo la wazi au kwa
ajili ya huduma za kijamii kama Manispaa wapo tayari kulipa fidia kwa
wananchi ili kupisha.
Hayo
ameyasema leo kwenye mkutano na wananchi wa mtaa wa Kunguru, kata ya
Goba wakiwa pamoja na taasisi binafsi inayijishughulisha na masuala ya
upangaji na upimaji wa maeneo nchini HUSEA.
Jacob
amesema, anatoa sifa kubwa sana kwa hatua iliyofikiwa na wananchi wa
Kunguru kwa kuamua kupima maeneo yao wenyewe na zaidi kwani Halmashauri
ndiyo wenye majukumu ya kufanya hivyo ila kwa hatua hiyo waliyofikia kwa
kushirikiana na HUSEA wamefanya jambo kubwa sana na wanawaunga mkono
kwa jitihada hizo.
"Kutakapotokea
kama kuna eneo ambalo ni eneo la wazi au kwa ajili ya huduma za kijamii
na limejengwa na mkakubaliana kupata eneo lingine kwa ajili ya shughuli
hizo basi msisite kutuambia kwani ili sisi kama Halmashauri tuweze
kulipa fidia, "amesema Jacob.
Mwenyekiti
wa HUSEA, Renny Chiwa amesema kuwa kwa hatua hii imeweza kusaidia
katika kupanga maeneo ya mtaa wa Kunguru na zaidi wananchi wameweza
kushirikiana nao kwa hatua nzuri mpaka kufikia kuweka makubaliano ya
upangaji wa maeneo na kuna baadhi ya wananchi wamejitolea kuacha maeneo
yao kwa ajili ya kuendeleza mipango endelevu.
Katika
eneo la Kunguru, kumeweza kupatikana kwa maeneo 1432 na wameweza
kuyapima na waliweza kupata ushirukiano mzuri kutoka kwa Wizara ya Ardhi
na waliweza kuwapa ramani halisi ya eneo hilo ila kutokana na wanachi
tayari wameshajenga wamepata sura ya ramani ambayo ni mpya na
itakapokamilikwa kupimwa kuanzia mwezi Januari mwakani watafanya
mabadiliko ya ramani hiyo.
Mkurugenzi
wa Mipango Miji na Vijiji, Prof John Lupala amesema kuwa wao kama
Wizara wamedhamiria kuhakikisha wanashirikiana na makampuni binafsi
kuweza kupima na kupanga maeneo ya makazi ya watu mjini na vijijini na
zaidi mpaka kufikia mwaka 2016 ni asilimia 15 tu ya maeneo yamepimwa.
Mradi huo
ulianza mnamo mwezi Mei mwaka huu na uliweza kupata changamoto
mbalimbali kutoka kwa wananchi ikiwemo watu kusema kuwa ni makampuni ya
kitapeli ila baada ya kuwapa elimu waliwez kuelewa na siku ya kwanza ya
mkutano huo wananchi zaidi ya 800 walijiandikisha kwa ajili ya kupimiwa
maeneo yao.(P.T)
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: