
RIPOTI YA MWAKA YA WHO KUHUSU MALARIA YALETA MATUKAINI
Posted by khamisimussa77@gmail.com at 11:38 AM
Ripoti ya
Shirika la afya duniani WHO kuhusu ugonjwa wa Malaria, inaleta
matumaini lakini wakati huo huo inatoa tahadhari kwamba ugonjwa huo bado
ni tishio kwa jamii hasa katika nchi zilizo Kusini mwa jangwa la Sahara
Kuna
habari njema kutokana na ripoti hiyo ya mwaka ya shirika la afya duniani
WHO kuhusu Malaria kwamba uwezekano upo wa kuutokomeza kabisa ugonjwa
huo kama matokeo yanavyoonyesha katika baadhi ya nchi. Mnamo mwaka 2015
nchi 10 na baadhi ya maeneo yaliripoti chini ya visa 150 vya ugonjwa wa
malaria. Nchi nyingine 9 ziliorodhesha kati ya visa 150 na 1000 kwa
ajili hiyo Shirika la Afya duniani WHO linaamini kuwa juhudi za
kuutokomeza ugonjwa huo japo katika nchi 10 zinaweza kufua dafu hadi
kufikia mwaka 2020.
Perdo
Alosno ni mkurugenzi wa WHO anayesimamia mpango wa kupambana na Malaria
anasema jambo la muhimu ili kupatikana kwa mafanikio na kuboresha huduma
za afya kwa watoto na akina mama wajawazito, hii ni pamoja na kuboresha
njia za kubainisha magonjwa na kutoa maelekezo ya tiba katika vituo vya
afya vya umma.
Na katika
hilo WHO inaweza kujivunia baadhi ya mafanikio. Dr. Alonso amesema,
kuna ongezeko la asilimia 77 katika kipindi cha miaka mitano kwa
wanawake wanaopata dozi tatu za kuzuia Malaria wakati wakiwa wajawazito
na pia kunaongezeko kubwa katika kueneza vyandarua vilivyonyunyiziwa
dawa kwa jamii ambayo inakabiliwa na hatari ya ugonjwa wa Malaria.
Mkakati
wa WHO wa kutokomeza Malaria unalenga kupunguza ugonjwa huo kwa asilimia
40 kufikia mwaka 2020. Hata hivyo nchi nyingi hazina uwezo wa
kupambana kikamilifu na Malaria. Ripoti ya Shirika la Afya duniani WHO
inaeleza kuwa nusu ya nchi 91 na maeneo yanayokabiliwa na ugonjwa huo wa
Malaria yanakaribia kulifikia lengo la kuungamiza ugonjwa huo. DW
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: