RC- KIGOMA AGIZA KIJIJI KIKAGULIWE URAIA WA WANANCHI MKOANI KIGOMA

NA MAGRETH MAGOSSO,KIGOMA


MKUU wa Mkoa wa  Kigoma Brigedia Jenerari Emanuel Maganga ameviagiza vyombo vya usalama vya hapo,wakague uraia wa wananchi waishio katika Kijiji Cha Matendo katani humo wilayani Kigoma kutokana na changamoto ya kugombea ardhi baina ya wakulima na wafugaji,ilihali awali  kila kaya walipatiwa  hekari 10 ya shughuli hizo.

Akitoa kauli hiyo kijijini humo,katika ziara ya siku moja ya kukagua miradi ya maendeleo na kuongea na wananchi wa vijiji kadhaa katika wilaya hiyo,iliyolenga kubaini kero zinazowakabili sambamba na hatua madhubuti ya kupunguza kero hizo,ambapo katika ziara hiyo ,ilihusisha baadhi ya wakuu wa idara ya afya,maji,elimu,mkurugenzi  Hanji Godigodi na mkuu wa   wilaya  hiyo Samson Angana.

Maganga alisema  anawasiwasi na uingiaji wa raia kutoka nchi jirani (BURUNDI) ambao wengi wanajishughulisha na kilimo na ufugaji na kuziagiza mamlaka husika zichukue hatua za kiutendaji ,kwa kuwa kipindi cha miaka sita kwa  kaya 1505 yenye wakazi 7,400  wafikie hatua ya kutishiana maisha  kitendo  kisichokubalika na serikali ya awamu ya tano Rais John Magufuli.

Akifafanua zaidi Maganga alieleza kuwa,kijiji cha matendo kimegubikwa na ubabe baina ya wananchi na viongozi wa vijiji ,ambapo kila mkutano wa kijiji lazima kuwe na vurugu ,wananchi kukaidi mikutano ya msingi hasa ya kupokea tarifa ya mapato na matumizi,ambazo  zinaweza zikatatuliwa kwa njia ya mazungumzo ikiwa wana uchungu wa maendeleo ya kijiji chao.

“isije ikawa kuna raia wa kigeni hapa,tafadhali ukijijua si raia wa taifa hili,ondoka bwana msituletee vurugu  hapa,nagiza vyombo vya usalama na mamlaka husika waanze mara moja kukagua kaya moja hadi nyingine ,haiwezekani msusie mikutano ya kijiji kwa kitu cha zaidi ya miaka mitano,mwenyekiti mnamchagua wenyewe na wote ni chama kimoja sitaki fujo” alisema Mkuu wa mkoa wa kigoma.

Awali Diwani wa Kata ya Matendo  Athuman Ntanyagala alifafanua kuwa kuwa  ardhi ya matendo imepimwa yote kupitia mpango wa matumizi bora ya ardhi  kuanzia mwaka 1988 hadi 1990 mpango ulikamilika na kipande wanachogombea wakulima na wafugaji katika ardhi kiliachwa bila matumizi lakini wafugaji walianza kutumia katika shughuli za ufugaji kiholela na ramani ipo ya kijiji hiki na kushauri itumike ili kuondoa kero ya uvamizi wa bwawa la Kikombe .

Awali Mwenyekiti wa wafugaji wa hapo  Masud Kibenda alidai wafugaji wanahaki ya kumiliki eneo hilo kwa kuwa walianza shughuli za ufugaji tangu mwaka tangu mwaka 1990 lakini likaja kundi la wakulima na kuanza shughuli za kilimo katika bonde la Kikombe hali iliyowafanya wakimbilie katika vyombo vya sheria na kushinda kesi mara kadhaa na kumuomba mkuu wa mkoa atoe tamko kwa wakulima .

Baadhi ya wananchi wa hapo kusikia tamko la ukaguzi wa uraia wa kaya moja hadi nyingine wakiomba hifadhi ya majina walisema `kwa hatua hiyo  wananchi wa matendo watabaki wachache kwa kuwa miongoni mwao wengi ni wakimbizi “.
Mwisho.

0 comments: