BREAKING NEWSS MADEREVA BAJAJI WAFUNGA BARABARA BAADA YA WENZAO 22 KUFIKISHWA MAHAKAMANI

Baada ya madereva 22 kufikishwa mahakamani vurugu kubwa zimezuka eneo la Block T jijini Mbeya baada ya vijana kufunga barabara hiyo kwa mawe na kuleta adha kubwa kwa watumiaji wa barabara.
Baadhi ya madeva wa Bajaj jijini Mbeya walofikishwa mahakama ya Wilaya ya Mbeya kwa kuvunja sheria za usalama barabarani ambapo jumla ya madereva 22 wamekamatwa na kufikishwa mahakamani. 
Uongozi wa Bajaj umesitisha huduma za usafiri wa Bajaj jijini Mbeya ili kujua hatma ya kesi ya wenzao na baadae kuanzisha vurugu zilizopelekea jeshi la polisi kuingilia kati na kuwadhibiti kwa mabomu ya machozi. (PICHA NA MBEYA YETU)

0 comments: