TANZIA

 Enzi ya uhai wake, John Paul Kazoka
UJIJIRAHAA blog ikishrikiana na Uongozi wa Taasisi ya Tiba ya Magonjwa ya Mifupa,   Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu  Muhimbili (MOI), kwa masikitiko makubwa kwa wafanyakazi wote na kipekee kwa wana fb wote kwa kifo cha mwenzetu John Paul Kazoka. kilichotokea chumba cha uangalizi Maalumu katika WD ya Mwaisela katika Hospitali ya Taifa Muhimbili alikokuwa amelazwa,  mwili wa marehemu ulisafirishwa 14/ 09/ 2016. kwenda Kijijini kwao Same , Chome Makanya  kwa ajili ya mazishi na kuzikwa 15/ 09/ 2016, ambapo kabla ya kusafirishwa marehemu  ibada ya kumuombea marehemu ilifanyika nyumbani kwao Mtoni Kijichi Jijini Dar es Salaam na Wafanyakazi, jamaa na marafiki na ndugu walipata nafasi ya kutowa heshima za mwisho. uongozi wa Taasisi hiyo iliandaa usafiri kwa waliokambatana na ndugu kuelekea Mtoni. Taasisi ya MOI, inashukuru kwa Madaktari na wauguzi  wote walioshirika katika kuokoa maisha ya mfanyakazi wake.  Mwenyeezimungu ilaze roho ya mpendwa wetu mahala pema peponi  (amina)

0 comments: