"SEGERA" LA CUF LAENDELEA, BARAZA KUU SASA LAMFUKUZA UANACHAMA PROFESA IBRAHIM LIPUMBA


CHAMA Cha Wananchi, CUF, kimetangaza kumvua uanachama wa Chama hicho, Mwenyekiti wake Profesa Ibrahim Haruna Lipumba ikiwa ni takribani siku tatu tu baada ya Ofisi ya Msajili wa vyama vya siasa nchini kumrejeshea uenyekiti wake ambao Baraza kuu la uongozi la chama hicho liliridhia barua yake ya kujiuzulu.
Kwa mujibu wa maafisa wa chama hicho, Baraza Kuu la Uongozi la CUF lililokutana visiwani Zanzibar juzi na Septemba, 27, 2016, limeamua kumvua uanachama Profesa Lipumba, kwa maelezo kuwa hatua hiyo ni muhimu katika kukinusuru chama hicho kisisambaratike
Kwa mujibu wa maafisa hao uamuzi wa Baraza Kuu la Uongozi la Taifa la CUF unatokana na uwezo wake kwa mujibu wa Katiba ya Chama, Ibara ya 10 (1)(c) limemfukuza uanachama Prof. Ibrahim Lipumba.
Hata hivyo Profesa Lipumba alikaririwa akisema, kikao cha Baraza Kuu la Uongozi kilichofanyiak Zanzibar hakikuwa halali kwa vile mwenye mamlaka ya kuitisha kikao hicho ni Katibu Mkuu wa chama ambaye ni Maalim Seif Shariff Hamad, ambaye kwa sasa yuko ng'ambo kwenye matibabu. "Kwa vile Maalim hayupo, mwenye mamlaka ya kuitisha kwa sasa ni Naibu Katibu Mkuu wa chama (Tanzania Bara), ambaye ni Magdalena Sakaya, lakini mama Sakaya hakuitisha kikao hicho, hivyo ni kikao batili kwa mjibu wa katiba ya chama." Alikaririwa Profesa Lipumba  Septemba 26, 2016 akisema

0 comments: