Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu Dar. Simon Sirro |
'PANYA ROAD' WAIBUKA UPYA NA KUTESA WANANCHI MOSHI BAA JIJINI DAR ES SALAAM
Posted by khamisimussa77@gmail.com at 9:00 AM
Na Dotto Mwaibale
KUNDI la uhalifu la watoto wenye umri
kuanzia miaka 18 hadi 25 maarufu kama panya road linatishia usalama wa
wananchi na mali zao maeneo ya Moshi Baa na vitongoji vingine katika
Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam.
Kufuatia kukithiri kwa vitendo hivyo
katika kipindi kisichopungua wiki mbili tayari watoto watatu walikuwa
wakidaiwa kuhusika na kundi hilo wameuawa na wananchi wenye hasira kali.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi
Dar es Salaa leo hii mkazi wa eneo la Moshi Baa Relini aliyejitambulisha
kwa jina la Mwarami Abubakar alisema hali sio shwari katika eneo
kufuatia matukio ya kila siku ya kuvamiwa wananchi kujeruhiwa na kuporwa
mali zao na kundi hilo.
"Tayari vijana wawili wiki iliyopita
wamechomwa moto na wananchi wenye hasira huku mwingine akipigwa juzi
hadi kutolewa utumbo na kufariki papo hapo" alisema Abubakar.
Mkazi mwingine wa eneo la Kwa Mkolemba
Khamisi Fadhil alisema kundi hilo limekuwa likifanya vitendo hivyo
mchana kweupe na wanatembea kuanzia vijana nane hadi 10 wakiwa na silaha
za jadi kama nondo, visu na mapanga na mtu yeyote wanayekutana naye ni
lazima wampige na kumpora.
"Wenye maduka wanalazimika kufunga
kuanzia saa moja jioni kuhofia kundi hilo ambalo huvunja milango ya
nyumba na kufanya uporaji" alisema Fadhil.
Fadhil alisema maeneo ambayo vijana hao wameshamiri ni Moshi Baa Relini, Kwa Mkolemba, Diwani na Bomba mbili.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi wa
Ilala, Kamishna Msaidizi (ACP), Salum Hamdan alisema polisi imejipanga
vilivyokukabiliana na vitendo hivyo katika mkoa wake.
"Kwanza napenda kukuambia kwamba hakuna
kundi linalojiita panya road wote tuna wahesabu ni wahalifu kama walivyo
wahalifu wengine na hivi ninavyongea na wewe tupo katika siku ya sita
ya operesheni ya kukakamta watu wanaojihusisha na uhalifu wa ujambazi
wakiwemo wanaouza pombe haramu ya gongo " alisema Kamanda Hamdan.
Aliongeza kuwa katika mkoa wake hivi
karibuni utakuwa shwari baada ya askari wake kusambaratisha watu hao
wanaofanya vitendo hivyo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: