MUSEVENI ATOA DOLA LAKI 2 KUSAIDIA WAATHIRIKA WA TETEMEKO LA ARDHI MKOANI KAGERA, MSAADA WA RAIS KENYATTA KUWASILI BUKOBA MUDA WOWOTE KUANZIA SASA
Posted by khamisimussa77@gmail.com at 1:23 PM
Waziri Mkuu
Kassim Majaliwa akisoma taarifa ya Tetemeko la ardhi lililotokea mkoani Kagera
Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifuatilia kwa
makini taarifa iliyokuwa ikitolewa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kuhusu
Tetemeko la ardhi lililotokea mkoani Kagera
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
John Pombe Magufuli akimshukuru Naibu Balozi wa Kenya hapa nchini Boniface
Muhia mara baada ya kupokea salamu za pole kutoka kwa Rais wa Kenya Uhuru
Kenyatta na kwa misaada mbalimbali ambayo inatarajiwa kuwasili mkoani Kagera kutoka
Kenya muda wowote
Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. John Pombe
Magufuli akimshukuru Balozi wa Uganda hapa nchini Doroth Samali Hyuha mara
baada ya kuwasilisha mchango wa kiasi cha fedha Dola za Kimarekani laki mbili (USD
200,000) kutoka kwa Rais wa Uganda Yoweri Museveni
Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea msaada wa fedha kiasi
cha dola laki mbili (USD 200,000) kutoka
kwa Balozi wa Uganda hapa nchini Doroth Samali Hyuha wapili kutoka (kushoto)
akiwa pamoja na Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Uganda Elibariki Maleko. Msaada
huo umetolewa na Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni kwa ajili ya kuwasaidia
wahanga wa Tetemeko la ardhi mkoani Kagera.
Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe
Magufuli akizungumza mara baada ya kupokea taarifa ya Tetemeko la ardhi
lililotokea mkoani Kagera kutoka kwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Ikulu jijini
Dar es Salaam.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: