Na Mathias Canal, Kilimanjaro
Wakulima wa mazao mbalimbali likiwemo zao la vitunguu wametakiwa kutofanya biashara kwa kujaza rumbesa ili kuwanufaisha wafanya biashara ambao wanajitokeza vijijini kunua mazao kwani jambo hilo linawanyonya zaidi wakulima na kuwanufaisha wafanya biashara.
Hata hivyo lengo mahususi la kuamua kuwapo kwa zoezi la upimaji ardhi ni kutaka kuondoa migogoro ya ardhi iliyokithiri katika maeneo mbalimbali Wilayani humo sambamba na kupinga kipimo cha Rumbesa kinachowanyonya wakulima wengi nchini.
Katika mkutano huo uliofanyika Katika Kitongoji cha Jitengeni na Mvungwe uliwahusisha pia wataalamu wa kilimo na ardhi kutoka katika Halmashauri ya Wilaya hiyo sambamba na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama katika Wilaya hiyo.
Katika mkutano huo Mkuu wa Wilaya hiyo aliwataka wakazi wa Kijiji cha Ruvu Jiungeni kushiriki kikamilifu katika zoezi la upimaji ardhi hivyo kuwaarifu pia wananchi wote kujitokeza katika mashamba yao wakati wa zoezi la upimaji ili kuondoa adha inayochochea migogoro kati ya wakulima na wafugaji.
Dc Staki alisema kuwa wananchi wanapaswa kupinga kuzidisha kipimo halisi kinachokubalika kwani kutofanya hivyo ni kukubali kupunjwa na kuinyima Halmashauri mapato.
Alisema kuwa wakulima wanapaswa kujiamini kwani mazao wanayolima yana soko popote nchini hivyo kidanganywa kwa kuweka Lumbesa ni kujinyima haki yao ya msingi katika kukabiliana na wimbi la umasikini.
Aidha kabla ya mkutano na wananchi Dc Staki alitembelea mashamba ya vitunguu na kujionea jinsi ambavyo Rumbesa inavyofungwa.
Sambamba na hayo pia Mkuu huyo wa Wilaya alimtaka mkuu wa Polisi Wilaya ya Same Asteriko Maiga kusimamia na kulikemea suala la Rumbesa kwenye mageti yote na endapo watawabaini wafanya biashara wanaofanya hivyo wanapaswa kukamatwa na kuchukuliwa hatua.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Same Anna-Claire Shija alisema kuwa wananchi wanapaswa kuwa makini katika kuimarisha kilimo na kujitokeza kwa wingi katika shughuli za maendeleo.
0 comments: