Mke
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli
akisalimiana na Baadhi ya Viongozi wa Serikali, Chama na Wazee wakati
akiwasili kwenye kituo cha kulea wazee cha Nkaseka kwa ajili ya kutoa
misaada ya Chakula, Mavazi pamoja na Vifaa vya Malazi.
Mke
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli
akisaini kitabu cha wageni baada ya kuwasili kwenye kituo cha kulea
wazee cha Nkaseka Mkoani Mtwara kwa ajili ya kutoa misaada ya Chakula,
Mavazi, Madawa pamoja na Vifaa vya Malazi.
Mke
wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Mary Majaliwa
akisaini kitabu cha wageni baada ya kuwasili kwenye kituo cha kulea
wazee cha Nkaseka Mkoani Mtwara
Kaimu
Afisa Mfawidhi wa Kituo cha kulea wazee cha Nkaseka Mkoani Mtwara Bw.
Rashidi Kambona akimkabidhi taarifa ya kituo hicho Mke wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli.
Mke
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli
akiongea na wazee katika kituo cha Nkaseka Mkoani Mtwara na kumshukuru
Mtumishi wa Mungu TB Joshua kuunga mkono juhudi zake za kuwasaidia wazee
na watu wasiojiweza kwa kuchangia baadhi ya vitu vilivyotolewa kama
msaada kwenye kituo hicho.
Muwakilishi
wa Mtumishi wa Mungu TB Joshua Nchini Tanzania akitoa salamu kutoka kwa
TB Mhandisi Consolata Ngimbwa Joshua aliyetoa msaada kwa ajili ya wazee
wa kituo cha Nkaseka kilichopo Wilayani Masasi Mkoani Mtwara.
Mke
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli
akimkabidhi Kiongozi wa Wazee wa Kituo cha Kulea Wazee cha Nkaseka .
Boniface Mbedo misaada jana Mkoani Mtwara.
Mke
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli
akifurahia jambo na moja ya Mzee wa Kituo cha Kulea Wazee cha Nkaseka
baada ya kumpa zawadi ya Ungo, Chungu na Mwiko. Kulia ni Mke wa Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Mary Majaliwa, wakati wa
hafla ya utoaji misaada kwenye kituo cha kulea wazee na watu wasiojiweza
cha Nkaseka Mkoani Mtwara.

0 comments: