WAFANYAKAZI wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kitengo cha Tekinolijia ya meno, wamempongeza Dk. Wilfred Lekule kwa kufikia hatamu kwenye utumishi wa umma kisheria na kuwa mfano wa kuigwa kwao.
Akisoma hutuba kwa niaba ya wanafunzi wahimu wenzake waliwahi kufundishwa na Dk. Lekule, Fundi Sanifu Meno Leonald Magea, alisema wakati wa utumishi wake wakati akiwa Mkuu wa Chuo cha Tekinolojia ya meno, licha ya kukutana na changamoto kadhaa lakini hakusita kutoa mchango wake kwa ajili ya kuendeleza taaluma hiyo chuoni hapo.
"Ulipokuwa Mkuu wa Chuo hiki, licha ya kukumbana na changamoto lukuki lakini hukisita katika utoaji wa elimu hapa chuoni hali iliyisaidia wanafunzi waliopitia hapa kupata elimu ambao kwa sasa wamekuwa wakiitumia katika kuhudumia jamii inayowazunguka katika sehemu zai kazi," alisema.
Aliongeza kuwa kutokana na jambo hilo bado wanaendelea kuthamini na kukumbuka mchango wa Dk. Lekule ambaye amestaafu kwa mujibu wa sheria na kukufanua kuwa wamehamasika kuandaa sherehe ya kumpongeza ili kukubali uwezo wake na mchango wake taaluma hiyo kwao.
Pia alisema licha ya kustaafu kwa Dk. Lekule katika utumishi wa Umma lakini bado mchango wake unahitajika katika kuihudumia jamii ipige hatua katika Tekinolijia ya meno ndani ya nchi na nje ya mipaka ya Tanzania.
Kwa niaba ya wenzake na kutambua mchango wake walimuomba Dk. Lekule kutosita kuendelea kutoa mchango wake kitaaluma kwa watu wa kada hiyo ambao bado wanahitaji msaada kutoka kwake licha ya kustaafu.
Pia Mkuu wa Chuo wa ambaye amepokea kijiti kutoka kwa Dk. Lekule, Dk. Gaudensia Mgoma aliahidi kufanya nyendo za mtangulizi wake kwa maana alikuwa kiungo muhimu baina ya wanachuo na jamii iliyopo chuoni hapo.
"Sitamwangusha na nimejifunza moyo wa uchapakazi, kwani wakati mwingine alikuwa akizidiwa na maradhi lakini alikuwa akifika chuoni na kupiga kazi hata mguu wake ulipokuwa umevimba haukumpa shida kutekeleza majukumu yake," alisema
mwisho.
0 comments: