Kiongozi wa kundi la Islamic State ambaye amehusishwa na shambulio la kigaidi la Paris Ufaransa ameuawa na majeshi ya muungano.
Jeshi la Marekani limesema kiongozi huyo Charaffe al Mouadan alikufa katika katika shambulio la anga.
Msemaji
wa jeshi la Marekani amesema mpiganaji wa Kisyria alikuwa akipanga
mashambulizi zaidi dhidi ya nchi za magharibi na alikuwa na mawasiliano
ya karibu na anayetuhumiwa kupanga shambulio la Paris.
Jeshi la Marekani limesema viongozi 10 wa Islamic State wameuawa mwezi huu
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

0 comments: