EWE MWANAADAMU ! NINI KIKUDANGANYACHO UKAMWACHA MOLA WAKO MLEZI MTUKUFU?

Ewe Mwanaadamu! Nini Kikudanganyacho Ukamwacha Mola Wako Mlezi Mtukufu?

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala)  
((يَا أَيُّهَا الْإِنسَانُ مَا غَرَّكَ بِرَبِّكَ الْكَرِيمِ))
((Ewe mwanaadamu! Nini kikudanganyacho ukamwacha Mola wako Mlezi Mtukufu?)) [Al-Infitwaar: 6]
  • Utukufu gani wa Mwenye maneno haya yenye kushtua nyoyo na kusisimua mwili?
  • Siku utakayoitwa "Ewe Mwanaadamu maskini uliye dhaifu, kitu gani kikudanganyacho?"
  • Nini kilichokughilibu hata ukamu'asi Mungu Mmoja (Pekee) Mwenye nguvu? (za mwisho)
  • Nini kilichokudanganya hata ukavuka mipaka ya Mola wako?
  • Nini kilichokudanganya hata ukapuuza Swalah?
  • Nini kilichokudanganya hata ukatenda maovu usiku na mchana?
  • Nini kilichokudanganya hata ukapeleka macho yako kutazama yalio haramu?
  • Nini kilichokudanganya hata ukawa humuogopi Mola wako kama unavyowaogopa viumbe vyengine?
  • Nini kilichokudanganya hata ukawa huna khofu ya kukutana na Mola wako na kuhesabiwa?
  • Je, ni dunia? Na Je? Hujui kama dunia ni nyumba ya kupita tu?
  • Au ni shahawaat (matamanio)?  Hujui kama nayo ni ya kuondoka?
  • Au ni Shaytwaan aliyekuhadaa? Kwani hujui kama yeye kwako ni adui mkubwa?
  • Basi ni kipi kilichokudanganya?  Jibu! Jibu! Ndugu Muislamu, leo kabla ya kesho kufika! Kwani hujijui kama utafika kesho kama alivyosema Mshairi: 

تزود من التقوى فإنك لا تدري                    إذا جن عليك ليل هل تعيش إلى الفجر
Zidisha taqwa  kwani hujui
usiku utakapokufunika, je, utaishi hadi Alfajiri?

فكم من صحيح مات بغير علة                  وكم من سقيم عاش حينا من الدهري
Kwani wangapi waliokuwa na siha zao wamekufa bila ya maradhi
Na wangapi walio wagonjwa wameishi miaka?

وكم من صغار يرتجى طولة عمرهم               وقد دخلت أجسادهم ظلمة القبر
Na Wangapi miongoni mwa wadogo wametumainiwa maisha marefu
Na miili yao imekwishaingia katika kiza cha kaburi

 
فكم من فتى يمسي ويصبح ضاحكا              وقد نسجت أكفانه وهو لايدري




Na vijana wangapi wameamka huku wanacheka
Kumbe huku sanda yao inashonwa/inaandaliwa naye hajui

وكم من عروس زينوها لزوجها                 وقد قبضت أرواحهم ليلة القدر
Na bi harusi wangapi  amepambwa kwa ajili ya mume wake
Na roho zao zimechukuliwa usiku wa Laylatul-Qadri?

وكم من ساكن عند الصباح بقصره                  وعند المساء قد كان من ساكن القبر




Na wangapi asubuhi walikuwa katika maqasri yao wakikaa
Na jioni yakawa makazi yao ni kaburi?

فكن مخلصا وأعمل الخير دائما                         لعلك تحظى بالمثوبة والأجر




Kuwa mwenye ikhlaas na utende mema daima
Huenda ukabahatika kupata thawabu na jazaa

 وداوم على تقوى الإله فإنها أمان                   من الأهوال في موقف الحشر

Na dumisha Taqwa ya Mola Wa Pekee kwani ni hifadhi
itakayokulinda na hali katika siku ya kukufuliwa

لا إله إلا الله ...                                  Laa Ilaah Illa
Ewe ndugu Muislamu imekuingia khofu ya kurudi kwa Mola wako na kuacha kuendelea kudanganyika?
Kumbuka madhambi yako na amka usiku ujikaribishe kwa Mola  Mtukufu Mwenye kusamehe madhambi na Mwenye Rahma na urudie hii Aayah mara kwa mara ili ingie katika moyo wako.  
  ((يَا أَيُّهَا الْإِنسَانُ مَا غَرَّكَ بِرَبِّكَ الْكَرِيمِ))
((Ewe mwanaadamu! Nini kikudanganyacho ukamwacha Mola wako Mlezi Mtukufu?)) [Al-Infitwaar: 6]

Ndugu Muislamu, tafakari matukio yaliyotajwa katika hii Surah Tukufu yatakayotokea siku ambayo hutoweza kujisaidia wala kusaidiwa!

  بِسْمِ اللّهِ الرَّحْمَنِ الرَّحِيمِ   
((إِذَا السَّمَاء انفَطَرَتْ)) ((وَإِذَا الْكَوَاكِبُ انتَثَرَتْ))  ((وَإِذَا الْبِحَارُ فُجِّرَتْ))   ((وَإِذَا الْقُبُورُ بُعْثِرَتْ)) ((عَلِمَتْ نَفْسٌ مَّا قَدَّمَتْ وَأَخَّرَت)) (( يَا أَيُّهَا الْإِنسَانُ مَا غَرَّكَ بِرَبِّكَ الْكَرِيمِ)) ((الَّذِي خَلَقَكَ فَسَوَّاكَ فَعَدَلَكَ)) ((فِي أَيِّ صُورَةٍ مَّا شَاء رَكَّبَكَ))

KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHMA MWENYE KUREHEMU

((Mbingu itapochanika)) ((Na nyota zitapotawanyika)) ((Na bahari zitakapopasuliwa)) ((Na makaburi yatapofukuliwa)) ((Hapo kila nafsi itajua ilichotanguliza, na ilichobakisha nyuma)) ((Ewe mwanaadamu! Nini kilicho kughuri ukamwacha Mola wako Mlezi Mtukufu?)) ((Aliyekuumba, Akakuweka sawa, Akakunyoosha)) ((Katika sura yoyote Aliyoipenda Akakujenga)) [Al-Infitwaar: 1-8]

0 comments: