MBUNGE
mteule wa Viti Maalumu Mkoa wa Singida, Aysharose Mattembe, amesema
ushindi wa kishindo wa Dk. John Magufuli, ni ishara kuwa watanzania
wanataka mabadiliko ya maendeleo na si bora mabadiliko.
Amesema
ana imani kubwa watanzania hawatajutia uamuzi wala kura zao
walizompigia Dk. Magufuli kwa kuwa, yote aliyoahidi yanakwenda kufanyiwa
kazi na hatimaye Tanzania kuwa ya tofauti katika muda mfupi ujao.
Aidha,
amesema uchaguzi umemalizika kwa amani na watanzania wamefanya uamuzi
sahihi hivyo, kilichobaki ni wote kuungana na kufanya kazi kwa bidii ili
kuleta mabadiliko yanayokusidiwa.
Aliyasema
hayo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari kutoa shukrani zake
kwa Watanzania na wananchi wa Singida kwa kumchagua Dk. Magufuli na
wagombea ubunge na udiwani wa CCM.
Alisema
wananchi wa Singida wameonyesha mshikamano mkubwa na ukomavu wa kisiasa
kwa kujitokeza kwa wingi kwenye mikutano ya hadhara kusikiliza sera na
baadaye kufanya uamuzi sahihi wa kuwachagua kwa kishindo wagombea wa
CCM.
“Niko
hapa kuwashukuru Watanzania wote kwa kufanya uamuzi sahihi wa kumchagua
mgombea urais wetu, Dk. John Magufuli kwa kishindo na hatimaye
kutangazwa kuwa mshindi.
“Uamuzi
waliofanya umetokana na CCM kusimamisha mtu makini, mwadilifu na mwenye
dhamira ya dhati ya kutuletea maendeleo ya haraka na ya kweli. Kazi
kubwa iliyopo mbele yetu ni kuungana na kufanya kazi kwa bidii kutimiza
ndoto za watanzania. Falsafa yetu ya HapaKaziTu ndiyo inakwenda
kutekelezwa sasa,” alisema Aysharose.
Mbunge
huyo mteule, ambaye amejizolea sifa na umaarufu mkubwa kutokana na
kupambana kikamilifu katika kusaka ushindi wa wagombea wa CCM katika
ngazi ya utais, ubunge na madiwani, alisema amejipanga kuhakikisha
anatatua changamoto zinazowakabili wanawake na vijana.
Alisema
wakati wa kampeni, alizunguka katika maeneo mbalimbali mkoani Singida
na huko alikutana na kero mbalimbali ambazo tayari ameanza kuzifanyia
kazi kabla ya kuwapishwa kuwa mbunge.
Aysharose
alisema changamoto ya huduma za afya na uwezeshaji kiuchumi kwa
akinamama na vijana ndiyo kitakuwa kipaumbele chake cha kwanza mara
baada ya kuapishwa.
“Nimeona
changamoto nyingi, lakini kwa kuanzia nitaweka nguvu katika huduma za
afya na uwezeshaji kiuchumi kwa wanawake ili kuwawezesha kukua kiuchumi.
Natambua kuwa ukimuwezesha mwanamke basi umewezesha familia nzima
kusonga mbele kimaendeleo na hili, nitalipa msukumo wa aina yake,”
alisema.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

0 comments: