ADO NOVEMBER MWENYEKITI WA SHIRIKISHO LA MUZIKI TANZANIA ASIFU NA KUPONGEZA UTENDAJI WA RAIS DK. JOHN POMBE MAGUFULI
Posted by khamisimussa77@gmail.com at 2:04 AM
Addo November Mwasongwe Rais Shirikisho la Muziki Tanzania
amekutana na waandishi wa habari huko Mlimani City jijini Dar es salaam
na kuzungumza nao November amesema kwamba
Kwa Sasa tunaongozwa na kauli Mbiu ya Hapa Kazi Tu hivyo ni
bora tukae Muda mfupi na kwenda kuchapa Kazi Tu na si kupoteza muda
mwingi hapa.
Amesema Ziara za Ghafla za
Ndugu Magufuli siyo za kubezwa Ni za kupongezwa sana. Japo kuna wenye
roho mbaya na wasioitakia mema nchi yetu wanabeza maana wao walizoea
kubweteka na kufurahia wanyonge wakiteseka.
Shirikisho la Muziki Tanzania
tumeona matunda ya Rais Magufuli juzi amekwenda Muhimbili na Jana
tangazo limetoka kuwa mashine za MRI zimeanza Kufanya Kazi hili jambo si
la kubezwa hata kidogo bila jitihada binafsi za Ndugu Magufuli leo
watanzania wangeendelea kufa na kukata tamaa kwa kukosa matibabu.
Haikuwa rahisi kwa wakati Kama
huu ambao Ni wa Kupanga serikali mpya bado Rais ametoa Muda wa kwenda
kuhakikisha wanyonge wanapata matibabu na huduma tuna pongezi sana Ndugu
Magufuli.
Tunasema Ziara hizo za
kushtukiza ziendelee ili azibe mianya katika maeneo mengi yenye mianya
ya wakwepa kodi hasa Kwenye madini ambako tuna Mikatana mibovu
iliyoingiwa na wasio na Huruma, wizi na usafirishaji haramu wa madini,
Ni Jambo la aibu Tanzanite kwa wingi ipo Kenya na Afrika Kusini na kodi
hatukupata ipasavyo na kwingine kwingi Kama Kwenye mbuga za wanyama na
utalii ambapo wanyama wanauwawa kwa Faida ya wachache Jambo hili ni la
kulivalia njuga na mengine mengi.. Kwa kuziba mianya hiyo na kuleta
maendeleo ya wote hakika hatutahitaji misaada ya wazungu.. Tupo tayari
kufunga Mkanda kwa miaka hii mitano ili kuacha hazina kwa Taifa letu
lenye kila aina ya utajiri.
Tunamtakia afya tele na
tunaahidi ushirikiano kwake Kwenye haki za wanamuziki Kama alivyotuahidi
pale Mlimani City vile vile Tunamuombea kwa Mungu apate Baraza la
Mawaziri dogo lenye ufanisi na kupunguza mzigo kwa serikali Kama dhamira
yake alivyoionesha Kwenye kuondoa safari za Nje vile vile Tunamuombea
kwa Mungu asiogope vitisho vya Chura Yeye anywe Maji. Maji Ni kuwaletea
maendeleo watanzania.
Hali hii ya kasi ya Magufuli
itawafanya Diasporas wote wakumbuke kuwekeza nyumbani maana Sasa wanajua
hazina zao zitakua salama maana mwadilifu anaongoza nchi. Naomba
nichukue nafasi hii kuwatoa hofu watanzania waishio ughaibuni kuwa nchi
ipo Salama na Dereva wetu kwa Sasa ni Makini kweli kweli.
Zaidi ya yote ninapongeza
wasanii wote walioshiriki Kwenye kampeni za vyama mbali mbali Sasa
kampeni zimeisha Ni Muda wa Kufanya Kazi tuwe wamoja.. Rais wetu Ni
Magufuli tuvunje Makundi kwani siasa siyo uadui Ni Muda wa kujiletea
maendeleo yetu wenyewe!
Tunaandaa Mkutano Mkubwa wa
Amani na Maandamano ya kuunga Mkono Hatua za Magufuli kwa kweli tuna
Imani naye na tunaamini Mungu atamuwezesha kuyatimiza yote na kukata Kiu
ya watanzania.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: