ASKOFU GWAJIMA APATA DHAMANA POLISI OYSTERBAY

Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima akiwa kwenye baiskeli ya wagonjwa wakati akitoka katika Hospitali ya TMJ Dar es Salam leo mchana kwenda Kituo cha Polisi cha Oyterbay kupewa dhamana.
Askofu Gwajima akiingia kwenye gari huku 'akiugulia' wakati akielekea kwenye kituo hicho kupewa dhamana
Baadhi ya waandishi wa habari wakitoka kituo cha Polisi Oysterbay kufuatilia 
habari hiyo.
Wachungaji wakibadilishana mawazo wakati wakimsubiri Askofu Gwajima apewe dhamana
Waumini wa kanisa hilo wakijiandaa kumpokea Askofu wao 
baada ya kupatiwa dhamana
waumini hao wakiwa kituoni hapo.
Waumini wa Kanisa la Ufufuo na Uzima wakiwa wamelizonga gari lililombena Askofu Mkuu wa Kanisa hilo, Josephat Gwajima, huku wakishangilia kwa kusema Yesu, Yesu... baada ya kupewa dhamana  katika Kituo cha Polisi Oysterbay Dar es Salaam leo mchana.
Waumini hao wakilipungia mkono gari lililomchukua 
Askofu Gwajima.

0 comments: