Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Uzima na Ufufuo, Josephat Gwajima amejisalimisha kituo cha polisi kati kuhojiwa juu ya kutoa lugha chafu dhidi ya Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Muadhama Polycarp Kardinali Pengo.
Hata hivyo, mapema leo Asubuhi, kipande cha sauti ya Gwajima kilisambaa katika mitandao mbalimbali ya kijamii kikidai kuwa Gwajima angejisalimisha Polisi Jumatatu kwa kuwa kwa sasa yupo Arusha na kuwataka waumini wake kufika polisi Jumatatu bila kufanya vurugu.
Haijafahamika mara moja sababu zilizomfanya mchungaji huyo Kujisalimisha leo Ijumaa.
Nimekuwekea Kipande hicho hapo chini ambapo Gwajima anajitetea ni kwa nini Alitumia lugha hiyo
0 comments: