

Katika
kaunti ya Nyeri nchini Kenya kuna tukio lililotokea jana March 26
ambapo watu waliokuwa wakiomboleza walichukua mwili wa mtu mmoja na
kwenda nao katika kituo cha Polisi cha Mkurueni wakidai Polisi walihusika na kifo cha mtu huyo.
Waombolezaji
hao walichukua mwili huo katika chumba cha kuhifadhia maiti Hospitali
ya Nyeri na kuandamana hadi kituo hicho kwa madai mwanaume huyo alipigwa
risasi na Polisi wa kituo hicho, walikutana na maafisa wa Polisi ambao
walijaribu kuwazuia lakini waliwashinda nguvu na kuweka jeneza kwenye
mlango wa kituo hicho na kuondoka.
Polisi
waliwarushia mabomu ya machozi ili kuwatawanya, baadaye walikubaliana
hali ikakaa sawa ambapo ndugu wa marehemu huyo walikubali kuuchukua
mwili na kwenda kufanya mazishi.
Kusikiliza story hiyo iliyoripotiwa na kituo cha K24KI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: