KIBAKA WA BODABODA AFA KWA KUCHOMWA MOTO DAR KWA KUIBA MKOBA
Posted by khamisimussa77@gmail.com at 11:18 AM
Wananchi
wenye hasira katika eneo la Mlimani City jijini Dar es Salaam, juzi
jioni walimchoma moto mwendesha bodaboda aliyekuwa amempakiza mwenzake
ambao wanadaiwa kumpora mkoba dada mmoja na kujaribu kukimbia.
Wawili
hao wakiwa kwenye harakati kukimbia wananchi hao waliwazingira ambapo
aliyepakizwa aliruka na kufanikiwa kukimbia lakini aliyekuwa akiendesha
alidhibitiwa na kupewa kipondo kikali na kuchomwa moto na bodaboda yake.
Picha na GPL
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: