Wanasheria kutoka Ulaya na Marekani wanaoiwakilisha Kampuni ya Uwekezaji ya VIP Engineering and Marketing Limited wameibua ukweli juu ya mgogoro unaoikumba Kampuni ya Kufua Umeme hapa nchini ya IPTL.
Katika kueleza ukweli huo, Wanasheria hao waliongozwa na maswali yafuatayo katika mahojiano maalumu na waandishi wa habari yaliyofanyika jijini Arusha leo.
Miongoni mwa maswali waliyoulizwa Wanasheria hao yalikuwa yanahusu mada zifuatazo:
1. Kueleza historia fupi ya mgogoro wa IPTL tangu ulivyoanza hadi sasa.
2. Kueleza msimamo wa VIP Engineering and Marketing Ltd kuhusu Akaunti Maalumu (Escrow Account) iliyokuwa Benki Kuu ya Tanzania (BoT).
3. Kueleza kwa nini Akaunti Maalumu (Escrow Account) ilifunguliwa Benki Kuu ya Tanzania.
4. Kama hisa za IPTL zingetolewa kwa mtu mwingine zaidi ya PAP, kwa mfano, Benki ya Standard Chartered; Je ni kweli kuwa mnunuzi yeyote wa hisa za IPTL angeweza kuwa na haki juu ya Escrow Account?
5. Baadhi ya wahisani wametangaza kusitisha kuunga mkono bajeti ya Serikali kwa kuwa wanaamini kwamba kuna ufisadi kwenye fedha zilizokuwa kwenye Escrow Account. Upi ni ushauri wao kwa serikali ya Tanzania juu ya suala hilo.
6. Je Benki ya Standard Chartered inayo madai yoyote dhidi ya IPTL na kwenye akaunti maalumu (Escrow Account).
7. Kama wanauamini mfumo wa mahakama za Tanzania
8. Nini msimamo wako kuhusu madai yanayotolewa eti kwamba Mahakama za Tanzania zinanuka rushwa.
9. Baadhi ya vyombo vya habari hapa nchini zimetangaza kuwa Benki ya Standard Chartered imefanikiwa kupata amri ya mahakama huko Uholanzi kukamata mali za VIP Engineering and Marketing Ltd zilizoko katika nchi hiyo. Je kuna ukweli juu ya taarifa hizo. Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com
TUTAWALETEA MAJIBU YA MASWALI HAYO KWA KIREFU NA KWA UFASAHA BAADAYE.
0 comments: