Posted by
khamisimussa77@gmail.com
at
7:26 AM
Meneja
wa Man Utd, Aloysius Paulus Maria van Gaal amesema ameshangazwa na
hatua ya wachezaji wake kuridhika na mabao matatu ambayo walikuwa
wakiongoza, na mwishowe walimaini mambo yamekwisha.
Louis
van Gaal amesema kutokana na kitendo hicho kikosi chake kilistahili
kuadhibiwa kutokana na wapinzani kuonyesha kujituma wakati wote na
mwisho wa dakika 90 lengo lao lilitimia kwa kuibuka na ushindi mkubwa wa
mabao matano.
Amesema
aliamini walivyoanza vyema katika mchezo uliopita dhidi ya QPR kutokana
na kuwa na wachezaji aliowasajili mambo yangeendelea kwa nidhamu ya
mchezo kama walivyocheza Old Trffortd, lakini matokeo yake wameambualia
aibu na sasa hana budi kujipanga upya kwa ajili ya mchezo ujao ambapo
watapambana na wagonga nyundo kutoka magharibi mwa jijini London West
Ham Utd.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

0 comments: