KATIBU
Mkuu Mstaafu wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Dar es Salaam Kapteni
Mstaafu Mohammed Ligora amewataka wanasiasa kuacha kulumbana juu aina ya
katiba kwani wenye maamuzi ya mwisho ni wananchi ambao watapiga kura.
Ligora
alisema hayo jana ikiwa ni siku chache baada ya kuonekana hali ya
sintofamu juu ya hatma ya katiba pendekezwa ambayo imesomwa na Mweyekiti
wa Kamati ya Uandishi Adrew Chenge.
Alisema
anapatwa na mshangao dhidi ya baadhi ya viongozi ambao wamekuwa
wakiendeleza malumbano kupitia vyombo vya habari huku wakitambua kuwa
wenye maamuzi ya mwisho dhidi ya aina ya serikali na mambo mengine ni
wananchi.
Kapteni
Mstaafu huyo alisema ni vema viongozi wa kisiasa pamoja na wale
wanaoitwa watetezi wa haki za wananchi kujikita katika harakati za
kujenga nchi hasa pale ambapo inaonekana kuwa Chama Tawala na Serikali
yake kimeshindwa kufanya vizuri.
“Napenda
kutoa rai kwa wanasiasa na wanaharakati kujitikita katika masuala
mengine yenye tija kwa nchi kwani hili la katiba muafaka wake upo chini
ya wananchi wenyewe ambao ndio wataamua kuwa katiba iwepo au la”,
alisema Ligora.
Katibu
Mstaafu huyo alisema jamii ya Kitanzania ina watu wengi ambao
wameelimika hivyo hawahitaji kufanyiwa maamuzi ambayo yanaweza kuwa na
maslahi kwa watu wengine ambao wanajiita wanasiasa.
Aliwataka
wananchi kufanya maamuzi ambayo yatakuwa yamezungukwa na utashi wao
bila kushurutishwa na mtu yoyote kwani nchi ya Tanzania ni ya kila
mtanzania bila kuangalia rangi, elimu na ukabila.
Kwa
upande mwingine Kapteni Mstaafu huyo alisema ni wakati wa vyama vya
siasa kuonyesha ushirikiano mkubwa ili kuweza kudumisha umoja, amani na
utulivu wa Taifa la Tanzania ambalo limejaliwa jamii yenye upendo.
Alisema
kasoro ambazo zimeonekana katika mchakato mzima wa kutengeneza katiba
zisiwe sababu ya kupelekea Taifa katika machafuko kwani madhara yake
yatakuwa ya muda mrefu kwa jamii ya Watanzania.
“Unajua
suala la kujitambua ni muhimu katika maamuzi ili kuhakikisha kuwa
maamuzi yote tunayofanya yanakuwa na weledi jambo ambalo mimi naamini
asilimia 80 ya watanzania inajitambua”, alisema.
0 comments: