Mkurugenzi wa Angels Moments inayoendesha Kampeni ya Mwanamke na Uchumi, Naima Malima akitoa hotuba ya ufunguzi wa kampeni
hiyo iliyofanyika mkoani mwanza hivi karibuni. Kampeni hiyo yenye lengo
la kuwawezesha kiuchumi wanawake wajasiriamali ambapo kampeni hiyo
itafanyika mkoani Tanga Mwezi Oktoba. Picha na Angels Moments.
Mshairi maarufu bibi sauda akitoa burudani ya mashairi yake adhimu kwa lugha ya kufurahisha na burudani kwa wanawake wajasiliamali katika kampeni ya mwanamke na uchumi jijini mwanza.
Mkuu wa Wilaya ya Ilemela ambaye alikuwa mgeni rasmi katika Kampeni ya Mwanamke na Uchumi iliyofanyika Mwanza, Mh. Amina Masenza akifurahia mashairi ya Bi. Sauda (hayupo pichani) katika kughani mashairi yake kwa lugha ya kiswahili.
Mtoa
mada maarufu Emiliani Busara akitoa mada na kufundisha biashara bora
kwa wajasiliamali jijini mwanza katika kampeni ya mwanamke na uchumi
zilizofanyika jijini mwanza hivi karibuni.
Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Mh. Amina Masenza akihutubia wanawake wajasiliamali katika ufunguzi wa semina za kampeni ya mwanamke na uchumi jijini mwanza hivi karibuni.
mjasiliamali mwenye ulemavu wa macho akiuliza swali kutoka kwa watoa mada katika kampeni ya mwanamke na uchumi mkoani mwanza.
Mkuu wa Wilaya ya ilemela Mh: Amina Masenza bidhaa za wajasiliamali katika moja ya mabanda ya wanawake
walioshiriki katika kampeni ya mwanamke na uchumi katika viwanja vya magomeni kirumba jijini mwanza.
Huduma za upimaji Afya zilitolewa kwenye kampeni ya mwanamke na uchumi inayotolewa na kampuni ya Angels Moments jijini mwanza hivi karibuni.
Balozi
wa kampeni ya mwanamke na uchumi, Linah Sanga akitoa burudani katika
ufunguzi wa kampeni ya mwanamke na uchumi mkoani mwanza.
Picha ya pamoja.
Baada
ya kutoa elimu juu ya mafanikio na ujuzi wa biashara na ujasiriamali
kwa wanawake wajasiriamali mkoani Mwanza, kampeni ya mwanamke na uchumi
inahamia mkoani Tanga ambapo wanawake na vijana zaidi ya 600 wanategemea
kupata elimu ya msingi juu ya ujasiliamali na fursa zilizopo na nidhamu
ya matumizi katika kuhifadhi fedha na mikopo.
“Sasa
tunahamia mkoa wa Tanga ambapo sasa mafanikio ya kampeni ya mwanamke na
uchumi tunayapeleka kwa wanawake wajasiliamali na vijana ambapo pamoja
na mambo mengine,tumefanya tathimini ya mkoa wa Mwanza imeonesha
mafanikio makubwa kwani mrejesho ni mkubwa na hamasa ni ya kutosha
ambapo wajasiriamali wanatuomba turudi tena, na hili ni jambo la kutia
moyo”Anasema Naima Malima Mkurugenzi wa Angels Moment waratibu wa
kampeni ya mwanamke na uchumi kwa wanawake wajasiriamali nchini.
“Unajua
mkoa wa Tanga unafursa nyingi sana,na jambo la kufurahisha ni kwamba
viongozi wengi wa mkoa huu ni wanawake kama mimi, ukianzia mkuu wa mkoa
na mkuu wa wilaya wote ni wanawake na wanajitahidi kuhakikisha
wajasiliamali wanasonga mbele ambapo pamoja na mambo mengine masuala
haya yatajadiliwa na kufundishwa na wataalamu na watoa mada hivyo elimu
ya ujasiliamali na fursa zilizopo, usimamizi binafsi wa fedha na uwekaji
akiba, afya bora na uchumi kwa akina mama na mwisho ni mwanamke na
rslimali ardhi tunategemea mada hizi zitafundishwa kwa usitaadi wa hali
ya juu na wakufunzi wetu” anasisitiza Mkurugenzi huyo.
Kampeni
ya mwanamke na uchumi mkoani Tanga inatazamiwa kuhudhuliwa na
wawezeshaji na wakufunzi maarufu kama ndugu Emiliani Busara na Bi. Tabu
Likoko kutoka taasisi ya WAMA ya jijini Dar es Salaam. Elimu sahihi juu
ya mada tajwa hapo juu zitatolewa ambapo wanawake wajasiriamali kutoka
wilaya za Tanga, Muheza, Mkinga na Pangani zitashiriki.
Kampeni hii ni ya pili kufanyika katika
mkoa wa Tanga,baada ya awali kufanyika mkoani Mwanza ambapo itapambwa
na Balozi wa kampeni ya mwanamke na uchumi Mwanamziki LINAH SANGA ambaye
ataburudisha na kutoa elimu kupitia mziki wake na wimbo maalumu wa
kampeni ya mwanamke na uchumi ambapo imepanga kufanyika terehe 10 na 11
mwezi ujao jijini Tanga.
0 comments: