DEREVA WA UDA AONJA ADHA YA TRAFIKI SIKUKUU YA MASHUJAA JIJINI DAR ES SALAAM LEO
Posted by khamisimussa77@gmail.com at 7:05 AM
Askari wa Usalama barabara akimsainisha faini dereva wa Uda lenye namba za usajili T 428 CVP, Richard Lyimo kwa madai ya kupita njia isiyoruhusiwa baada ya kufungwa kwa ajili ya kupita viongozi waliokuwa wakielekea kwenye Maadhimisho ya Siku ya Mashujaa yaliyofanyika viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es Salaam leo. Hata hivyo abiria waliokuwemo kwenye daladala hilo walimlalamimkia askari huyo kwa kumtoza faini dereva huyo bila ya kuwa na kosa. Baada ya sekeseke hiloT daladala hilo liliruhusiwa kuondoka.
Na Khamisi Mussa
Leo asubuhi kulikuwa na tukio lililozua tafrani kati ya abiria waliokuwa wamepanda basi la Uda lenye namba za usajili lililokuwa likitokea Kivukoni kwenda Mnazi Mmoja kupitia mtaa wa Makunganya baada ya kukamatwa na askari wa usalaam barabrani bila ya dereva kuwa na kosa lolote.
Baada ya askari huyo kulikamata basi hilo alimsainisha dereva huyo faini ambapo alimuambia hakuwa naye na kuomba faini hiyo ailipe baadae.
Askari huyo alimruhusu kuondoka lakini katika hali iliyowashangaza wengi askari huyo aliwapigia simu wenzanke na kuwaeleza kuwa dereva huyo alikuwa amemkimbia ambapo alikamatwa na kuweka mahabusu tangu asubuhi hadi saa tisa arasili alipoachiwa baada ya kulipishwa faini ya sh.30,000.
Dereva huyo na kondakta wake Asheri Mbilinyi baada ya kuachiwa alimtaarifu mmiliki wa mtandao huu tukio zima lilivyokuwa.
Jitihada za kuwapata wahusika kwa upande wa Polisi ili kuzungumzia suala hilo hazikuzaa matunda.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: