Je waasi wa M23 watakoma?

Waasi wa M23 wakekuwa wakihangaisha wananchi Mashariki mwa DRC tangu Machi mwaka 2012
Dalili za kukaribia kushindwa kwa waasi wa M23 nchini DRC, ni ishara ya mabadiliko ya kisiasa na mpangilio wa kijeshi ambayo yanaweka wazi matumaini ya amani katika nchi hiyo kubwa na ambayo imekuwa na migogoro kwa miaka mingi.
Waasi wa M23 Mashariki mwa nchi, wamepata pigo kubwa katika wiki chache zilizopita , na kulazimisha kiongozi wao Bertrand Bisimwa kutoa amri ya kusitisha vita na kutaka mazungumzo ya amani kuanza tena nchini Uganda

0 comments: