MEYA SILAA AJA NA KAMPENI KABAMBE YA KUCHANGIA MADAWATI KUPITIA SANAA Inbox x
Posted by khamisimussa77@gmail.com at 8:18 AM
Mstahiki Meya wa Manispaa ya
Ilala Mhe Jerry Silaa (wa pili kushoto) akizungumza na waandishi wa
habari leo asubuhi kuhusu kampeni ya ‘Dawati ni Elimu’ kupitia wasanii
mbalimbali wa kuchora nchini. Kulia kwake ni Msanii Robin Mtila na
Kushoto ni Meneja Mkuu wa Hyatt Regency Kilimanjaro, Trevor Saldanha na
Mustafa Hassanali Mratibu wa Kampeni hiyo.
Meneja Mkuu wa Hyatt Regency
Kilimanjaro, Trevor Saldanha akizungumzia mchango wa hoteli yake katika
kampeni ya Dawati ni Elimu yenye kauli mbiu ya "Kalisha mmoja boresha
Elimu".
Mchoraji Robin Mtila akizungumza kwa
niaba ya wasanii wenzake ambapo ameelezea umuhimu wa sekta ya Elimu
katika fani ya sanaa nchini.
Mkurugenzi wa Advert Construction Ltd
Dhmy Jog akizungumza na waandishi wa habari baada ya kampuni yake
kuchangia Tsh 10 milioni kwenye kampeni hiyo ya kuondoa tatizo la
madawati katika shule za msingi na sekondari nchini.
Baadhi wasanii watakaoshiriki kwenye tamasha kubwa la Sanaa lenye lengo la kuchangia kampeni ya Dawati ni Elimu.
Mkutano na waandishi wa habari ukiendelea.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala
Jerry Silaa akiwa katika picha ya pamoja na wasanii wa Sanaa ya Uchoraji
pamoja na baadhi ya wadhamini wa kampeni hiyo.
.Kampeni ya Dawati ni Elimu yakusanya Tsh 1bilioni mpaka sasa lengo ni kufikia Tsh 4.98bilioni
.atoa wito kwa watanzania kujitokeza kwa wingi siku ya tamasha la mwaka dawati ni elimu
Na Moblog Team
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Mhe
Jerry Silaa akishirikiana na Hyatt Regency Kilimanjaro Hotel na wasanii
kumi maarufu nchini wameandaa tamasha kubwa la sanaa la mwaka kwa
wasanii wa kuchora (Painters) lenye lengo la kuchangia kampeni ya
“Dawati ni Elimu” katika shule za msingi na sekondari jijini Dar es
Salaam. Moblog linaripoti
Akizungumza na waandishi wa habari leo
jijini Dar es Salaam, Mhe Silaa amesema kuwa katika kampeni hiyo ya
‘Dawati ni Elimu’ kupitia programu ya (Annual Mayors Charity Ball)
wameamua tarehe 16 ya mwezi Novemba kuwa na tamasha la sanaa ya uchoraji
itakayowashirikisha wasanii kumi maarufu nchini.
“kwenye tamasha la tarehe 16 mwezi
Novemba mwaka huu wasanii wa kuchora wataweza kuchora picha mbalimbali
kwa ubunifu wao na kuweza kuonyesha kazi zao pamoja na kuuza kwa wateja
katika Hoteli ya Hyatt Regency Kilimanjaro Hotel na sehemu ya mapato
yatachangia madawati na asilimia zingine itakuwa faida yao baada ya
mauzo kwenye maonyesho ya picha ,” amesema
Amesema kuwa katika tamasha hilo la
sanaa ya kuchora wasanii wataweza kuonyesha kazi zao za sanaa katika
harakati za kuhamasisha jamii kuchangia kupunguza tatizo la madawati
kwenye shule za msingi na sekondari kupitia kauli mbiu ya “Kalisha
mmoja, boresha elimu”
Silaa aliongeza pia kwamba katika
tamasha hilo la mwaka pia kutakuwa na chakula cha mchana kwa wageni wote
wataohudhuria Shughuli hiyo ambayo itakuwa ya wiki nzima katika
kuhakikisha lengo hilo la kupata madawati kwenye shule linafanikiwa.
Amesema kuwa kwa sasa takwimu
zinaonyesha asilimia 30 ya wanafunzi wa shule za msingi na sekondari
wanakaa chini kwa kukosa madawati katika shule nyingi za kata mkoa wa
Dar es Salaam.
Alisisitiza kuwa ofisi yake kwa
kushirikiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Ilala wanatafuta njia
bora ambayo wachangiaji wanaweza kuchangia kupitia mitandao ya simu ili
kuhakikisha wananchi wote wanapata fursa hiyo adhimu na pesa za
wananchi zinafanya kazi iliyokusudiwa.
“watanzania ni lazima waamke ili
waweze kuchangia maendeleo ya elimu nchini katika kusukuma mbele maslahi
mapana ya nchi kwa siku za usoni ili taifa letu liweze kuwa na wananchi
waliopata elimu bora na si bora elimu,” alisisitiza Mhe Silaa
Kwa upande wake Meneja Mkuu wa Hyatt
Regency Kilimanjaro, Trevor Saldanha amesema kuwa ni sehemu ya mpango wa
hoteli hiyo kurudisha faida wanayopata kwenye jamii ili kusaidia
kupunguza matatizo na changamoto mbalimbali katika sekta ya elimu.
“Ni muhimu kwa wafanyabiashara
kushirikiana na jamii inayoitumikia na tutaendelea kusaidia jamii katika
siku za usoni tukiwa kama sehemu ya jamii husika,’ amesema
Naye Mkurugenzi wa Advert Construction
Ltd Dhmv Jog amesema kampuni yake inatambua umuhimu wa sekta ya elimu
kwa manufaa ya mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla katika kufuta ujinga.
Amesema kampuni yake kupitia kitengo
chake cha kusaidia jamii kimetoa Tsh 10milioni katika kusaidia kampeni
hii ya “Dawati ni Elimu” ili kupunguza na kuondoa kabisa tatizo la
madawati mashuleni
Wasanii wataopata nafasi ya kuonyesha
kazi zao za sanaa ya kuchora ni Robin Mtila, Aggrey Mwasha, Salum Kambi,
Cathbert Mkocha, Haji Chilonga, Tobias Miza, James Haule na Victor
Malulu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)






0 comments: