mwakilishi kutoka
shirika la hifadhi la nyanda za juu kusini Godwell ole meing`ataki wa pili
kushoto akiwa na waziri kivuli wa maliasili na utalii mbunge Peter Msigwa
ambae alikuwa mgeni rasimi leo katika maadhimisho ya Tembo Duniani
Hawa
ndio waliofika kumsikiliza mbunge Msigwa leo uwanja wa historia wa
Mwembetogwa ambao kawaida huwa anajaza umati wa watu ila leo patupu
Wananchi
wa jimbo la Iringa mjini wakimsikiliza mbunge Msigwa
mwakilishi kutoka
shirika la hifadhi la nyanda za juu kusini Godwell ole meing`ataki kushoto
akiwa na waziri kivuli wa maliasili na utalii mbunge Peter Msigwa ambae
alikuwa mgeni rasimi leo katika maadhimisho ya Tembo Duniani
waigizaji wakiigiza jinsi majangili wanavyofanya
ujangili
magari
ya wadau waliofikia kumsikiliza mbunge Msigwa leo
KWA mara ya kwanza mbunge wa jimbo la
Iringa mjini mchungaji Peter Msigwa amevunja rekodi ya kuhotubia wananchi
wachache kuliko mihadhara mbali mbali aliyopata kuifanya katika uwanja wa
Mwembetogwa mjini Iringa .
Uwanja huo ambao ni uwanja wa Histori kwa
mbunge Msigwa kupata wasikilizaji wengi jana amejikuta akiambulia patupu
baada ya idadi ya watu waliofika kumsikiliza kufika idadi ya chini ya 30
jambo ambalo limezua maswali mengi zaidi.
Pamoja na kuwa mhadhara huo wa leo
haukuandaliwa na Chadema bali ulilenga kuadhuimisha siku ya Tembo Duniani
ila bado kwa kiasi mvuto wa maadhimisho hayo yamepoteza mwelekeo
.
Baadhi ya wadau waliozungumza na mtandao
huu wamedai kuwa waandaaji wa maadhimisho hayo ya siku ya Tembo Duniani ndio
ambao wamefanya maadhimisho hayo bila kujiandaa na ndio sababu ya wananchi
kupuuza kufika uwanjani hapo.
Kwa upande wake mbunge Msigwa alimtaka
Rais Jakaya Kikwete kuwachukulia hatua wale wote wanaotajwa kujihusisha
na ujangili wa meno ya tembo ambao waziri wa maliasili na utalii amekuwa
akieleza umma kuwa watu hao wanajulikana .
Msigwa aliwataka wananchi wa nyanda za juu
kusini kufichua majangili wa meno ya tembo ili kuendeleza utalii na kujipatia
kipato.
Kauli hiyo ameitoa leo wakati wa maadhimisho
ya kupinga uuaji wa tembo dunuani ambayo yamefanyika mkoani Iringa yenye kauli
mbiu inayosema pinga ujangiri,na kubainisha kuwa utalii bila tembo hakuna
utalii.
"Napenda kutoa rai kwa kupitia hadhara hii
kumshinikiza Raisi wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Mrisho
Kikwete, kwa dhamana aliyopewa kwa kupitia katiba, aweze kuwafikisha mbele ya
vyombo vya dola na kuwatendea ipasavyo watuhumiwa wote wa ujangili hasa wa
tembo....Natoa shinikizo hili kwa kuwa mara kadhaa, mawaziri wenye dhamana
wameendelea kukiri kuwa wanawafahamu majangili mpaka sehemu wanazokaa lakini
imeendelea kuwapa muda. Swali la kuuliza, je tunasubiri tembo watoweke ndio
tuanze kumtafuta mbaya/mchawi wetu? Ama ndo msemo wa waswahili kuwa 'La kuvunda
halina ubani?'"
Msigwa alisema kuwa
moja kati ya maazimio katika maadhimisho ya siku ya tembo ni pamoja na kumtaka
Raisi kuwachukulia hatua maafisa na watendaji wote wa Serikali na vyombo vya
usalama ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakishukiwa na kushutumiwa kwa ushiriki
wao hasa katika kulinda ama kusaidia mtandao wa ujangili nchini.
Alisema kuwa Rais Kikwete hana budi
kulichukulia jambo hili la ujangili wa tembo kwa uzito mkubwa na kulipa nafasi
katika moja ya mambo ya msingi ambayo kama Taifa lazima tuyazungumze bila
kificho wala kulinda maslahi ya watu wachache tena kwa uwazi na ukweli kwa
kushirikiana na umma wa watanzania.
"Mapambano
dhidi ya ujangili na ukatili wa tembo lazima yafanywe kwa dhamira ya dhati na si
kwa nia ya kuwapumbaza wananchi huku watu waliopo katika mtandao wa ujangili
wakilindwa na kujinufaisha kwa maslahi yao "
Hata hivyo alisema hadi sasa ni dhahiri
kuwa ukimya wa Serikali na kigugumizi chake cha kuwachukulia hatua watuhumiwa
kunatokana na ubinafsi, uozo na kutojali maslahi ya taifa kwa
ujumla.
"...Napenda kuwahakikishia waandaji kuwa ,
nitaendelea kuwa mstari wa mbele katika kulinda rasilimali hizi muhimu na urithi
huu mkubwa wa taifa letu kwa moyo wangu, nafsi yangu,nguvu zangu na akili zangu
kwa kushirikiana na watanzania wote kwa ujumla bila kujali tofauti za kiitikadi
na misimamo...ningependa kuongea mengi, ila kwa leo napenda kumalizia kwa
kuwakumbusha wananchi pamoja na mashirika yasiyo ya kiserikali kuendelea
kutimiza wajibu wake wa kulinda haki za wanyamapori hasa tembo hata pale
tunapoona kuwa Serikali inafanya jitihada hafifu katika mambo ya
msingi.
kwa upande wake
mwakilishi kutoka shirika la hifadhi la nyanda za juu kusini Godwell ole
meing`ataki amesema kuwa Serikali inachangia billion 11 katika kuendeleza
miradi ya wananchi kama maji elimu,miradi ya kijamii na na kimazingira ambayo
fedha hizo zinatoka katika mfuko wa utalii na
maliasili.
Meing`ataki amewaomba wananchi pia kuwafichua
wmajangiri wa tembo ili kusaidia watalii waweze kuja nchini na kujipatia kipato
ili nchi iweze kuendeleza miradi ya kijamii.
Serikali kwa kutimiza wajibu wake wa kudhibiti
biashara haramu ya wanyamapori ni lazima pia mashirika yasiyo ya kiserikali
kuendelea kuongeza juhudi zao kuhakikisha kuwa elimu kutolewa kwa umma ili
kuongeza nguvu ya pamoja katika masuala ya kulinda wanyamapori.
0 comments: