HUDUMA YA TRENI YA JIJI YASITISHWA KWA MUDA BAADA YA KICHWA CHA TRENI KUPATA AJALI!
Posted by khamisimussa77@gmail.com at 9:09 AM
Uongozi wa Kampuni ya Reli Tanzania
(TRL) Unasikitika kuwaarifu Wakazi
wa Jiji na Wananchi kwa ujumla kusitishwa huduma treni ya Jiji ( Dar- Ubungo
Maziwa) kwa siku ya leo ya Alhamis Oktoba 03, 2013. Hatua hiyo imechukuliwa
kufuatia ajali ya kichwa cha treni hiyo kugongwa na lori jana Oktoba 2, 2013
saa 12:30 jioni katika makutano ya reli
Buguruni.
Ajali hiyo imesababisha kuharibika kichwa
cha treni na kuhitaji matengenezo kabla ya kuendelea na huduma. Uongozi wa TRL
unaahidi kusimamia matengenezo kwa wakati ili huduma za treni za Jiji zirejee
mapema kesho Ijumaa Oktoba 04, 2013. Kufuatia ajali hiyo hakuna mtu
aliyejeruhiwa zaidi ya lori kupinduka na kuharibika kichwa cha
treni.
Imetolewa na Afisi ya Uhusiano
,
Kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji
Mhandisi Kipallo Amani
Kisamfu,
Dar es
Salaam
Oktoba 03, 2013.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

0 comments: