ASASI YA TREE OF HOPE YAFUNGUA KLABU YA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA KATIKA SHULE YA SEKONDARI YA NGUVUMALI ILIYOPO JIJINI TANGA

Mkurugenzi wa Asasi ya Tree of Hope, Fortunata Manyaresa (wa pili kushoto), akimkabidhi cheti  Diwani wa Kata ya Nguvumali iliyopo jijini Tanga, Sele Boss baada ya  kushiriki mafunzo ya kupinga vitendo vya ukatili wa jinsia katika hafla ya kufungua klabu ya kupinga vitendo hivyo katika Shule ya Sekondari ya Nguvumali mjini humo. Kushoto ni Ofisa wa Polisi Jamii Mkoa wa Tanga, Mrakibu wa Polisi Sarah Komba na kulia ni Mkuu wa shule hiyo Grace Shemdoe.
Diwani wa Kata ya Nguvumali jijini  Tanga, Sele Boss akimkabidhi cheti cha ushiriki wa mafunzo hayo, Mkuu wa shule hiyo Grace Shemdoe.
Diwani wa Kata hiyo Sele Boss akimkabidhi cheti, mwalimu wa shule hiyo Roda Kagongo.
Hapa akimkabidhi cheti mwanafunzi Celina Mashaka
Mwanafunzi Peter Chamabi akikabidhiwa cheti cha ushiriki mafunzo hayo.
Wanafunzi wa shule hiyo wakiwa kwenye hafla hiyo.
Maofisa wa Asasi isiyo ya kiserikali ya Tree of Hope wakiwa kwenye hafla hiyo.
Wanafunzi wa shule hiyo wakiwa makini kuandika mambo yote yaliyokuwa yakifundishwa kuhusu ukati wa kijinsia.
Ofisa wa Polisi kutoka dawati la jinsia kituo cha Polisi cha Chumbageni, Frank Kipengele akitoa mada kwa wanafunzi. Kulia ni Mkurugenzi wa Tree of Hope na Ofisa Jamii Polisi Mkoa wa Tanga , Mrakibu wa Polisi, Sarah Komba.
Mwanafunzi Mariam Erasto akielezea ukati wa jinsia wanaofanyiwa na walimu wanaofanya mapenzi na wanafunzi wa shule hiyo.
Maofisa wa Treeof Hope wakiwa kwenye hafla hiyo.
Maofisa wa Afya wakimchukua damu mwanafunzi kwa ajili ya kumpima HIV ikiwa ni moja ya kazi iliyofanyika wakati wa ufunguaji wa klabu hiyo shuleni hapo.
Diwani wa Kata hiyo Sele Boss( kulia), akihutubia wanafunzi hao (hawapo pichani)
Wanasheria wa Asasi hiyo Gabriel Kitungutu (kulia) na Warehema Kibaha (katikati), wakiwa makini kuandika yale yote yaliyokuwa yakizungumzwa katika mkutano huo. Kushoto ni Mkuu wa Shule hiyo Grace Shemdoe. Wengine nyuma ni maofisa wa Asasi hiyo.
Wanafunzi wakiwa na mabango yanayotoa elimu ya kupinga ukatili huo.
Maofisa wa Tree of Hope wakiwa kwenye hafla hiyo.
Wanafunzi 25 wa shule hiyo wakionesha vyeti vya kushiriki mafunzo ya kupinga ukatili wa jinsia walivyo kabidhiwa na Asasi hiyo.

0 comments: