Amos Makala afungua rasmi Maonyesho ya Wiki ya Vijana Kitaifa mkoani Iringa leo


Picha na 1 Naibu Waziri wa Habari, Vijana ,Utamaduni na Michezo Amos Makala akizungumza na wakazi wa manispaa ya Iringa wakati wa ufunguzi rasmi wa Maonyesho ya Wiki ya Vijana Kitaifa yanayofanyika mkoani  Iringa. Kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Iringa Dkt. Christine Ishengoma na Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Vijana Bw. James Kajugusi. Picha na 2Mkurugenzi wa Idara ya  Vijana kutoka  Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bw. Kajugusi akitoa ufafanuzi  kuhusu Maonyesho ya Wiki ya Vijana yanayofanyika kila mwaka nchini wakati wa Kumbukumbu ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru na kuwataka vijana kutumia fursa za kiuchumi zilizopo kujiletea maendeleo. Picha na 3Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Amosi Makala akiwa ameambatana na mkuu wa mkoa wa Iringa Dkt. Christine Ishengoma wakiangalia banda la Maonyesho la vijana wajasiriamali kutoka Zanzibar wanaoshiriki Maonyesho ya Wiki ya Vijana mkoani Iringa.
Picha na 4Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Amos Makala akiangalia gari lililotengenezwa kwa kutumia mbao na vifaa vya asili na mbunifu Keny Joseph kutoka kijiji cha Nyororo, Mufindi. Gari hilo ambalo limekua kivutio kikubwa katika maonyesho hayo analitumia katika shughuli zake za kila siku na lina uwezo wa kusafiri umbali wa kilometa 180 kwa saa. Picha na 5Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Amosi Makala akiingia ndani ya gari hilo. Picha na 6Sehemu ya mbele ya gari hilo ambalo limewavutia vijana wengi wakati wa maonyesho ya wiki ya vijana mkoani Iringa kama inavyoonekana huku mbunifu wa gari hilo Bw. Keny Joseph (kushoto) akirekebisha baadhi ya vitu katika gari lake. Picha na 7Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Amos Makala akipata maelezo kuhusu mifumo ya kompyuta katika banda la VETA mkoa wa Iringa wakati wa Maonyesho ya wiki ya Vijana kitaifa yanayofanyika katika viwanja vya Mlandege manispaa ya Iringa. Picha na 8Mkuu wa Mkoa  wa Iringa Dkt. Christine Ishengoma (kulia) na Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Vijana Bw. James Kajugusi wakitazama na kuonyesha kuvutiwa na  baadhi ya bidhaa zilizokuwa katika banda la maonyesho la Vijana wa mkoa wa Dar es salaam. Picha na 9 Mkurugenzi Ustawi wa Jamii,Maendeleo ya Wanawake, Vijana na Wanawake kutoka Zanzibar Bw.Mohamed Salim Alli akifungua mdahalo wa Vijana wakati wa Wiki ya Vijana katika Ukumbi wa VETA mkoani Iringa Picha na 10Vijana wakishiriki mdahalo wa wazi wa Wiki ya Vijana , Kumbukumbu ya Mwalimu Julius Nyerere , Mbio za Mwenge wa Uhuru na Fursa za uwekezaji zinazopatikana katika mkoa wa Iringa leo katika ukumbi wa VETA Iringa.
Picha na Aron Msigwa- MAELEZO.

0 comments: