WATU 18 WAHOFIWA KUFA KATIKA AJALI YA KUNIKWA NA KIFUSI JIJINI ARUSHA.
Posted by khamisimussa77@gmail.com at 7:57 AM
---
Inakadiliwa
watu zaidi ya watu 18 wamepoteza maisha kufuatia kufukiwa na gema la
mchanga/moram wakati wakichimba na kupakia kwenye malori eneo la Moshono jijini
Arusha.
Shuhuda
mmoja wa ajali ambae pia ni mchimbaji ameieleza Blog hii kwamba kwa kawaida
gari ndogo kama Fuso hupakiwa na watu 7, na hiyo kubwa huwa na watu 12 bila
kuhesabu dereva na utingo.
Miongoni
wa waliofikwa na mauti ni pamoja na madereva wa magari hayo. Katika eneo la
ajali hali ni ya simanzi na vilio toka kwa kina mama huku baadhi wa wababa na
marafiki na ndugu wa jamaa waliofukiwa wakishindwa kujizuia na kuangua
kilio.
Meya wa
Manispaa Mh Gaudence Lyimo pamoja na Mbunge wa Arusha Mjini Mh Godbless Lema ni
miongoni mwa viongozi wakubwa waliofika eneo la ajali kusaidiana na kikosi cha
Jeshi la Wananchi wa Tanzania kufanya uokozi.
Wachina
wakipeleka moja ya mashine zao (Excavator) kuongeza nguvu katika kusaidia
kufukua miili ya watu hao iliyonaswa na kifusi
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: