WATAKIWA KUBORESHA MISHAHARA NA UTENDAJI KWA WATUMISHI
Posted by khamisimussa77@gmail.com at 10:13 PM
NA MAGRETH KINABO – MAELEZO
KAIMU
Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma,HAB
Mkwizu amewataka wajumbe Bodi ya Mishahara na Masilahi katika
Utumishi wa Umma, kuwa na uhusiano na ushirikiano endelevu utakaolenga
kutoa ushauri mzuri kwa bodi na serikali ili kuboresha mishahara na
utendaji katika utumishi huo.
Kauli hiyo ilitolewa leo(jana) na Katibu Mkuu huyo wakati akifungua
mkutano wa siku mbili wa bodi hiyo unaohusisha wakuu wa idara, vitengo
vya utawala na usimamizi wa rasilimali watu kutoka utumishi huo
unaofanyika hoteli ya Blue Pearl jijini Dares Salaam.
“Wakati
wa kujadili suala hili, itabidi kuangalia kwa kina ili muone jinsi ya
kutumia nafasi zenu kutumia mifumo iliyopo ili kuhakikisha kuwa masihali
na tija havitenganishwi aua lugha nyingine haki na wajibu
vinaunganishwa ipasavyo,” alisema Mkwizu.
Katibu
Mkuu huyo alisisitiza kuwa kama masilahi hayataendana na tija yatakuwa
si endeleavu na yanaweza kuwa chnazo cha migogoro kati ya serikali na
wanayakazi, hilo likitokea huduma zitasimama na nchi itakuwa kwenye
tatizo la kutotoa huduma.
Alisema mkutano huo utakuwa na tija iwapo wajumbe watatoa michango na mapendekezo yao ambayo yatasaidia bodi kuishauri serikali.
Aidha alisema kwa kipindi kirefu kumekuwa na malalamiko mengi katika
utumishi na misingi yake pamoja na sababu nyingine ni tofauti ya kipato
au kile kinachooneka kama ni mgawanyo usio wa haki wa rasilimali za
taifa.
Mkwizu
aliongeza kuwa michango hiyo iwe endeleavu na bodi ianzishe
utaratibu/mfumo wakupokea michango toka wa wadau na hasa kwa wao
wenyewe.
Jumla ya
mada sita zitajadiliwa katika mkutano huo, ambazo ni muundo na majukumu
ya bodi, uhusinao na masilahi ya bodi, nafasi ya wakuu wa idara za
utawala na usimamizi wa rasilimali watu katika kuboresha masilahi, hali
ya uchumi na mwenendo wa mishahara, gharama za maisha na hali ya
mishahara nchini na kupitia rasimu ya dodoso la kukusanya taarifa za
gharama za maisha na hali ya mishahara.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: