MWENYEKITI WA WAMA MAMA SALMA KIKWETE AKABIDHI MSAADA WA VIFAA TIBA VYENYE THAMANI YA SHILINGI MILIONI 700 KWA HOSPITALI KUU YA MKOA WA RUKWA
Posted by khamisimussa77@gmail.com at 10:10 PM
Mke
wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA), Mama
Salma Kikwete akimkabidhi Mganga Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Dr. John Gurisha
orodha ya vifaa mbalimbali vya tiba kwa ajili ya hospitali ya Mkoa wa
Rukwa tarehe 26.2.2013 hospitalini hapo. Vifaa hivyo vimeletwa nchini na
Taasisi ya WAMA kwa kushirikiana na Kampuni ya Project C.U.R.E kutoka
Marekani na vina thamani ya shilingi milioni mia saba.
Mke wa Rais na
Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA), Mama Salma
Kikwete akimkabidhi Mganga Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Dr. John Gurisha moja
ya vifaa mbalimbali vya tiba kwa ajili ya hospitali ya Mkoa wa Rukwa
tarehe 26.2.2013. Baadhi ya vifaa hivyo ni mashine za Ulta Sound, X-Ray,
Upasuaji, tiba ya macho, tiba ya kinywa na meno, mgongo, mifupa,
mashine ya dawa za usingizi, vitanda maalum (TCU beds) n.k. Kushoto
anaeshuhudia makabidhiano hayo ni Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella
Manyanya.
Baadhi ya
vifaa tiba alivyokabidhi Mke wa Rais na Mwenyekiti wa WAMA Mama Salma
Kikwete vikiwa na thamani ya shilingi milioni mia saba. Vifaa hivo
pamoja na vingine ambavyo bado vipo kwenye kontena vimeletwa nchini na
Taasisi ya WAMA kwa kushirikiana na Kampuni ya Project C.U.R.E kutoka
Marekani.
Mama Salma
Kikwete akiongea na wadau wa sekta ya afya na wananchi waliokusanyika
katika viwanja vya hospitali kuu ya Mkoa wa Rukwa muda mfupi kabla ya
kukabidhi vifaa tiba kwa hospitali hiyo vyenye thamani ya shilingi
milioni mia saba.
Mkuu wa Mkoa
wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya akimkaribisha Mama Salma Kikwete
kuzungumza na wadau wa afya katika viwanja vya hospitali kuu ya Mkoa wa
Rukwa ambapo alikabidhi vifaa tiba kwa hospitali hiyo vyenye thamani ya
shilingi milioni mia saba. Mkuu huyo wa Mkoa alimshukuru Mama Salma kwa
jitihada anazozifanya yeye na taasisi yake katika kuunga mkono juhudi za
Serikali kuboresha huduma za afya nchini, alimuhakikishia kuwa Serikali
yake ya Mkoa itahakikisha inasimamia vizuri sekta ya afya kutimiza
ahadi za Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi 2010-2015 ambazo ni
pamoja na kuimarisha huduma za afya nchini.
Katibu wa Taasisi ya
Wanawake na Maendeleo (WAMA) Daudi Nasib akielezea kwa kifupi kazi na
majukumu ya taasisi hiyo kwa wadau wa afya waliohudhuria hafla fupi ya
makabidhiano ya vifaa tiba kutoka WAMA kwa uongozi wa hospitali kuu ya
Mkoa wa Rukwa. Miongoni mwa malengo makuu ya taasisi hiyo ni kuimarisha
afya ya mama na mtoto na kuunga mkono juhudi za Serikali katika
kuboresha huduma ya afya nchini.
Ndugu Abdul Kimario wa shirika la Project
C.U.R.E kutoka Marekani ambae shirika lake limeshirikiana na WAMA
kuleta vifaa tiba hivyo hapa nchini akitoa ufafanuzi wa matumizi ya
baadhi ya vifaa hivyo kwa wadau wa afya waliokusanyika kushuhudia
makabidhiano hayo.
Mama Salma Kikwete
akimkabidhi Mzee Protas Kimario kitambulisho cha matibabu ya uzeeni
kuwakilisha wazee wengine 458 zoezi lililoenda sambamba na kukabidhi
vifaa vya tiba kwa Hospitali Kuu ya Mkoa wa Rukwa tarehe 26.02.2013.
Jumla ya vitambulisho 4356 sawa na asilimia 96% katika Manispaa ya
Sumbawanga vimeshatengenezwa kwa ajili ya matibabu ya wazee.
Mama Salma Kikwete akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Iddi Hassan Kimanta funguo za pikipiki kwa
ajili ya vituo vya afya vya Wilaya hiyo katika jitihada za kuzuia
maambukizi ya virusi vya ukimwi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto
(PMTCT). Jumla ya Pikipiki kumi kutoka Water Rid zilikabidhiwa kwa ajili
ya huduma hizo katika Mikoa ya Rukwa na Katavi.
(Picha na Hamza Temba – Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa)
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: