ANATAFUTA NDUGU ZAKE

Anayeonekana pichani ni kijana aliyepokelewa Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI) akiwa hajitambui, baada ya kupata ufahamu amejitambulisha kwa jina la Selemani Kondo anakadiriwa kuwa na umri wa miaka 25, anadai kuwa mkazi wa Mbagala Maji Matitu .Tangu alipolazwa mpaka taarifa hii inapotoka hakuna hata ndugu mmoja aliyejitokeza.
Hivyo Uongozi wa Taasisi ya Mifupa (MOI) unaomba ndugu zake wajitokeze popote walipo na kumchukua ndugu yao ambaye amekwisharuhusiwa. selemani Kondo amelazwa katika Taasisi ya Mifupa (MOI) WODI 2B,
"Selemani alipokelewa hapa MOI katika mapokezi ya dharura akitokea Hospitali ya Amana akiwa hajitambui mnamo tarehe 19 Januari 2018. Mpaka sasa hivi ameanza kujitambua, ametoa jina lake na kusema kwamba anatoka Mbagala Maji Matitu. Tunaomba ndugu na jamaa zake waje kumchukua kwani amekwisharuhusiwa". Amesema Bwana Jumaa Almasi, Meneja Ustawi na Uhusiano wa Taasisi hiyo.(PICHA NA KHAMISI MUSSA)

0 comments: