Na Bashir Nkoromo, Kigamboni.
Wanawake
wajasiliamali wametakiwa kutengeneza au kuuza bidhaa zenya ubora wa
viwango vinavokubalika ili kuvutia wateja kununua bidhaa zao na kuongeza
masoko ndani na nje ya Nchi.
Hayo yamesemwa leo na Mkurugenzi wa Uhuru FM Angel Akilimali
ambaye alikuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa Jukwaa la Wanawake Kata ya
Somangila, Manispaa ya Kigamboni jijini Dar es Salaam.
Katika uzinduzi huo uliofanyika Uwanja wa Dege katika Kata hiyo
Angela alisema mbali na na bidhaa bora kuhamasisha wanunuzi na kuongeza
masoko ndani na nje ya Nchi boa bidhaa hizo zinaweza kumudu ushindani
katika soko.
Alivishauri vikundi vya Wanawake wajasiliamali kwenda kuomba
mikopo kwenye Benki ya Wanawake Tanzania ambayo alisema ni benki yenye
mikopo ya riba nafuu.
Uzinduzi wa Jukwaa hilo ni sehemu ya shamrashamra za Maadhimisho
ya Siku ya Wanawake Duniani ambayo yatafanyika mapema mwezi huu.
Wanawake
wa vikundi vya Wajasiriamali wakiandamana kutoka kwenye Ofisi yao
kwenda kwenye uwanja wa Dege, kwenye Uzinduzi wa Jukwaa la Wanawake wa
Kata ya Somangila Wilayani Kigamboni, Dar es Salaam, leo
Mgeni
rasmi kwenye uzinduzi wa Jukwaa la Wanawake Kata ya Somangila,
Kigamboni Dar es Salaam, Kaimu Mkurugenzi wa Uhuru FM Angel Akilimali
(kulia) akiwa na baadhi ya Viongozi wa Jukwaa hilo wakati wakipokea
maandamano ya Wanawake Wajasiriliamali kwenye uzinduzi wa Jukwaa hilo,
leo
Viongozi
wa Vikundi mbalimbali vya Wanawake Wajasiliamali na Jukwaa la Wanawake
wakiwa tayari kupokea maandamano ya wanawake Wajasiriamali. Kushoto ni
Mgeni Rasmi Kaimu Mkurugenzi wa Uhuru FM angel Akilimali akipunga mikono
Viongozi wakimwayamwaya kupokea maandamano hayo
Mgeni
rasmi Kaimu Mkurugenzi wa Uhuru FM Angel Akilimali akisoma moja ya
mabango waliyokuwa nayo Wanawake Wajasiliamali walipowasili Uwanjani
kwenye uzinduzi wa Jukwaa la Wanawake Kata ya Somangila.
Diwani
wa Kata ya Somangila Wilayani Kigamboni, Francis Chichi (kulia)
akionyesha umahiri wa kusakata muziki pamoja na Kinamama wakati wa
Uzinduzi wa Jukwaa la Wanawake wa Kata hiyo, leo
Mwanamke
Mjasiliamali wa kutengeneza vifaa vya ujenzi Amina Zakumera (kushoto)
akimpatia maelezo ya utaalam wake Mgeni Rasmi Kaimu Mkurugenzi wa Uhuru
FM Angel Akilimali (Wapili kulia) alipokuwa akikagua bidhaa za Wanawake
wajasiriamali wakati wa uzinduzi wa jukwaa la Wanawake wa Kata ya
somangila, Kigamboni, leo
Angel
Akilimali akipata maelezo kuhusu bidhaa za mwanamke mjasiliamali
Winifrida Jafari (kushoto) wakati wa uzinduzi wa Jukwaa la Wanawake wa
Kata ya Somanga, Kigamboni leo. Wapili kushoto ni Mjasiriamali Joha
Amour wa Joha Fashion.
Angel Akilimali akitazama mkeka uliotengenezwa na Mwanamke Mjasiriamali Jawa Maulidi (kushoto)
Angel Akilimali (kushoto) akimuuliza Mwanamke mjasiliamali jinsi anavyotengeneza bidhaa zake.
Angel
Akilimali na Diwani Chichi wakinywa togwa kwenye banda la maonyesho la
Mwanamke Mjasiliamali, wakati wa uzinduzi wa Jukwaa la Wanawake wa Kata
ya Somangila, Kigamboni.
Wanawake wajasriamali wa Kata ya Somangila wakijimwayamwaya kucheza muziki kufurahia uzinduzi wa Jukwaa lao, leo
Mtendaji
wa Kata ya Somangila Munna Msafiri akitambulisha viongozi wa vikundi
mbalimbali na Jukwaa la wanawake kutoka maeneo mbalimbali
Viongozi wa Majukwaa ya Wanawake kutoka kata mbalimbali za Halmashauri ya Kigamboni wakitambulishwa
Diwani
wa Kata ya Somangila Ndugu Chichi akifanya harambee ya uchangiaji wa
fedha kutunisha mfuko wa Jukwaa la wanawake katika kata yake.
Mkuu wa Polisi Kata ya Somangila Mwakila Chile akizungumza baada ya kutambulishwa na Diwani Chichi
Mwekezaji
wa Mbutu Beach Resort katika Kata ya Somangila Prakash Naran akiungana
na Wanawake wajasiliamali kusakata muziki wakati wa sherehe za uzinduzi
wa Jukwaa la Wanawake Kata ya Somangila
Mwekezaji
wa Mbutu Beach Resort katika Kata ya Somangila Prakash Naran akicheza
ngoma na msanii wa kikundi cha Vijana wa Somangila wakati wa Sherehe
hizo za uzinduzi wa Jukwaa la Wanawake Kata ya Somangila
Mgeni
rasmi katika Sherehe za uzinduzi wa Jukwaa la Wanawake Kata ya
somangila Kigamboni Angel Akilimali akifurahia vijana walivyokuwa
wakionyesha uhodari wa kucheza sarakasi wakati wa sherehe hizo
Kijana akiwa kihwa chini miguu juu, tena hewani wakati akicheza sarakasi wakati wa sherehe hizo
Wasani wa kikundi cha sanaa cha Vijana wa Smangila wakionyesha uhodari wa kucheza sarakasi wakati wa sherehe hizo
Mgeni
rasmi katika sherehe za Uzinduzi wa Jukwaa la wanawake wa Kata ya
Somangila, Kigamboni, Angel Akilimali akinadi kiatu alipoendesha mnada
wa vitu mbalimbali vya wanawake wajasriamali wakati wa sherehe hizo
Mwekezaji
wa Mbutu Beach Resort katika Kata ya Somangila Prakash Naran
akikitazama kwa makini kiatu hicho baada ya kukubali kukinunua kwa sh
50,000
Angel Akilimali akihutubia Wakati wa Sherehe za uzinduzi wa Jukwaa la Wanawake wa Kata ya Somangila, Kigamboni, leo
Angel Akilimali akihutubia Wakati wa Sherehe za uzinduzi wa Jukwaa la Wanawake wa Kata ya Somangila, Kigamboni, leo
Angel Akilimali akipongezwa na MC katika sherehe hizo
Angel
Akilimali akiwa na mtunza Fedha wa Jukwaa la Wanawake Kata ya Kigamboni
Pili Doto mwishoni wa uzinduzi wa Jukwaa la Wanawake kata ya Somangila
Angel Akilimali (kulia) akizungumza jambo na Mkurugenzi wa New Life Queen Bahati mwishoni mwa sherehe hizo
Angel Akilimali akiwa na baadhi ya Wanawake wajasiliamali
Mgeni
Rasmi katika sherehe za uzinduzi wa Jukwaa la wanawake Kata ya
Somangila, Kigamboni Dar es Salaam, Angel Akilimali akiwa katika picha
ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Jukwaa hilo katika kata mbalimbali za
Kigamboni na Viongozi wa vikundi vya Wanawake wajasiriamali wa kata
hiyo baada ya uzinduz leo. (PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO)
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: