Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, ameondoka nchini leo, tarehe 07 Oktoba 2026, kuelekea Doha, Qatar. kwa ziara ya kikazi inayolenga kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi na kufunguwa fursa mpya za maendeleo kwa Zanzibar
read moreLatest Articles
RAIS DR. MWINYI AANZA ZIARA YA KIKAZI QATAR NA HISPANIA KUFUNGUA FURSA MPYA ZA UWEKEZAJI
Posted by khamisimussa77@gmail.com at 8:51 AMMAKAMU WA RAIS KUFUNGUA MKUTANO WA 46 WA CATA JIJINI ARUSHA
Posted by khamisimussa77@gmail.com at 9:33 AM
Makamu wa Rais amewasili kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA), ambako amepokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. CPA Amos Gabriel Makalla, pamoja na viongozi wengine wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Serikali.
Mkutano huo utafanyika katika Ukumbi wa Grand Melia jijini Arusha na unatarajiwa kuwakutanisha viongozi na wataalamu zaidi ya 400 kutoka mataifa 48.
read more
RAISI MWINYI AAFUNGUA MKUTANO WA JUKWAA LA MAJAJI WAKUU WA NCHI ZA KUSINI NA MASHARIKI MWA AFRIKA (SEACJF. )
Posted by khamisimussa77@gmail.com at 9:04 AMAmesisitiza umuhimu wa ushirikiano wa kimahakama wa kikanda katika kuimarisha mifumo ya utoaji haki, kubadilishana uzoefu na kuhakikisha Mahakama zinaendana na mabadiliko ya teknolojia pamoja na mahitaji ya wananchi.
Ameelezea pia kuwa Mahakama zinapaswa kukumbatia ubunifu na teknolojia katika kuboresha huduma za haki, huku zikilinda misingi ya haki, usawa na taratibu stahiki za kisheria.
Aidha, amehimiza umuhimu wa kuwa na uhuru wa kifedha wa Mahakama, kwa kuhakikisha zinapata rasilimali za kutosha na zinazotabirika ili ziweze kutekeleza kwa ufanisi majukumu yao ya kikatiba.
Katika hafla hiyo, amezindua nyaraka tatu muhimu za Jukwaa la Majaji Wakuu wa Nchi za Kusini na Mashariki mwa Afrika (SEACJF).
Mkutano huu umewakutanisha Majaji Wakuu na viongozi wa Mahakama kutoka nchi 15 za Afrika kujadili ubunifu, ufanisi na mageuzi katika usimamizi wa Mahakama na utoaji wa haki.
Ninaamini kupitia ushirikiano huu, tutazidi kuimarisha mifumo yetu ya haki na kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora, kwa wakati na kwa kuzingatia misingi ya haki na usawa.

![]() |
. BAADA ya kupata wito kutoka kwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan wa kulitumikia Taifa kupitia uteuzi wa kuwa Mkuu wa Wilaya Arumeru, Neema Lugangira ameamua kusitisha mkataba wake wa kazi wa Katibu Mkuu wa Tassisi ya Viongozi wa Kisiasa Wanawake Duniani (WPL).Akizungumza baada ya kuapishwa kuwa Mkuu wa Wilaya hiyo Oktoba 3, 2026 jijini Arusha, Lugangira amesema kuwa amepokea dhamana aliyopewa na Rais Samia kwa unyeyekevu mkubwa na yuko tayari kushirikiana na wananchi na viongozi wote kuhakikisha malengo ya serikali yanafikiwa.
"Nimeupokea kwa unyenyekevu mkubwa uteuzi wa Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa DC Arumeru. Kwa hatua hiyo, nimeomba ofisi yangu iliyopo Brussels nchini Ubelgiji kukatisha mkataba wangu wa Katibu Mkuu WPL, na nimerejea nchini na kuanza kazi."
"Kwanza kabisa namshukuru Mwenyezi Mungu kwa fursa hii. Pia namshukuru sana Mhe. Rais Dkt. Samia kwa uteuzi alionipatia wa kumsaidia kwenye wilaya yetu ya Arumeru, " amesema Lugangira.
Amesema dhamira yake ni kuhakikisha wananchi wa Arumeru wanapata viongozi wanaowasilikiza, wanaowafikia na wanachukua hatua katika kutatua changamoto zinazowakabili.
read more
Jana tarehe 03 Oktoba 2026, katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika Ikulu Zanzibar, nimetangaza uteuzi na uhamisho wa Mawaziri na Naibu Mawaziri, pamoja na mabadiliko ya miundo ya baadhi ya Wizara.Mabadiliko haya ni sehemu ya kukamilisha uundwaji wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa, kwa kuwajumuisha Mawaziri kutoka ACT-Wazalendo, sambamba na kuendelea kutekeleza makubaliano ya maridhiano baina ya CCM na ACT-Wazalendo.
Katika uteuzi huo,
ACT-Wazalendo imepata nafasi nne za uwaziri:
• Mhe. Nassor Ahmed Mazrui – Waziri wa Afya.
• Mhe. Omar Said Shaaban – Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda.
• Mhe. Dkt. Nasra Nassor Omar – Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale.
• Mhe. Dkt. Mohamed Ali Suleiman – Waziri wa Mawasiliano, Teknolojia ya Habari na Ubunifu.
Aidha, nimefanya mabadiliko ya miundo ya baadhi ya Wizara, ikiwemo kuhamishia masuala ya Mipango katika Ofisi ya Rais, Ikulu, pamoja na kuanzisha Wizara ya Kazi, Ajira, Vijana na Uwezeshaji.
Katika mabadiliko hayo:
• Mhe. Shaaban Ali Othman – Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Ikulu, anayeshughulikia Mipango na Usimamizi wa Utendaji Serikalini.
• Mhe. Masoud Ali Mohamed – Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Ikulu, anayeshughulikia Uhusiano wa Jamii.
• Mhe. Mudrik Ramadhan Soraga – Waziri wa Uchumi wa Buluu na Uvuvi.
• Mhe. Ali Suleiman Ameir Mrembo – Waziri wa Kazi, Ajira, Vijana na Uwezeshaji.
Pia, nimefanya mabadiliko katika nafasi za Naibu Mawaziri katika Wizara mbalimbali, ikiwemo Afya, Kilimo, Elimu, Biashara na Maendeleo ya Viwanda, Fedha, Utalii na Mambo ya Kale, pamoja na Kazi, Ajira, Vijana na Uwezeshaji.
Mabadiliko haya yana lengo la kuimarisha ufanisi wa Serikali na kuendelea kutekeleza kwa vitendo makubaliano ya maridhiano yaliyofikiwa baina ya CCM na ACT-Wazalendo katika uundwaji wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa.
Mawaziri na Naibu Mawaziri wote walioteuliwa na waliohamishwa wataapishwa Jumatatu, tarehe 05 Oktoba 2026, saa 8:00 mchana.
Tunaendelea kujenga Zanzibar yenye umoja, utulivu na maendeleo kwa wote.
read moreSALAMU ZA RAMBIRAMBI KUTOKA OFISI YA MAKAMU WA RAIS KUFUATIA KIFO CHA MAMA FATMA KARUME
Posted by khamisimussa77@gmail.com at 3:53 AMKatika kipindi hiki kigumu cha majonzi na maombolezo, ninawaombea wafiwa wote faraja, subira na nguvu za kustahimili pengo kubwa lililoachwa na mpendwa wetu.
Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi, amjalie pumziko la milele na awape moyo wa subira wote walioguswa na msiba huu mkubwa.
“Inna lillahi wa inna ilayhi raji’un.”
Deogratius Ndejembi
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Angellah Jasmine Mbelwa Kairuki (Mb.), amewasili jijini New York, Marekani, kushiriki katika Mkutano wa 81 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UNGA81), pamoja na mikutano mbalimbali ya kimataifa inayofanyika pembezoni mwa mkutano huo.
Akiwa New York, Waziri Kairuki anashiriki katika Jukwaa la Siku ya Ushirikiano wa Kidijitali 2026 (Digital Cooperation Day 2026), lenye kaulimbiu “Shaping a Global AI Future Through Science, Policy, and Capacity.” Jukwaa hilo linawakutanisha viongozi wa Serikali, wadau wa teknolojia, wataalamu na washirika wa maendeleo kujadili namna ya kujenga mustakabali wa kidijitali na Akili Unde (AI) unaojumuisha na kunufaisha nchi zote.
Katika jukwaa hilo, Tanzania itashiriki katika meza ya majadiliano ya Mawaziri, itakayojikita katika hatua za kuimarisha ulinzi na usalama wa Miundombinu ya Umma ya Kidijitali (Digital Public Infrastructure – DPI), pamoja na mijadala kuhusu maendeleo na matumizi ya Akili Unde (Artificial Intelligence – AI) na teknolojia ya Tokenization.
Ushiriki wa Tanzania utatoa pia fursa ya kuwasilisha mwelekeo na mtazamo wa nchi kuhusu maendeleo, usimamizi na matumizi salama na yenye tija ya Akili Unde, hususan katika kuchochea maendeleo ya kiuchumi na kijamii na kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi.
Aidha, Tanzania itatumia jukwaa hilo kuangazia fursa na changamoto zinazolikabili Bara la Afrika katika zama za AI, ikiwemo mahitaji ya miundombinu ya kidijitali, uwezo wa kompyuta kwa ajili ya AI (AI computing capacity), upatikanaji na matumizi salama ya data, ukuzaji wa ujuzi wa kidijitali na AI, pamoja na uwekezaji na rasilimali fedha zinazohitajika kuwezesha nchi za Afrika kushiriki kikamilifu katika uchumi wa kidijitali duniani.
Ushiriki huo unalenga pia kuhimiza sauti na ushiriki wenye maana wa nchi za Afrika katika mijadala na maamuzi ya kimataifa kuhusu AI, hususan katika uundaji wa sera na mifumo ya usimamizi wa teknolojia hiyo, ujenzi wa uwezo wa kitaalamu, pamoja na uwekezaji katika miundombinu muhimu ya kidijitali.
read more
















.jpg)
.jpg)













.jpg)
.jpg)











