MELI ZA JESHI LA IRAN ZATIA NANGA KATIKA BANDARI YA DURBAN

Meli za kikosi cha upelelezi cha operesheni ya mabaharia 44 wa jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, zimewasili katika bandari ya Durban, Afrika Kusini.
Meli hizo zinazozijumuisha meli ya ulinzi na meli ya Alvand zinaelekea bandari ya Cape Town na bahari ya Atlantic nchini Afrika Kusini. Kwa mujibu wa habari, balozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Ira nchini Afrika Kusini, Mohsen Movahedi Ghomi amezipokea meli hizo katika bandari hiyo ya Durban nchini humo.
Sehemu ya msafara wa manwari za Jamhuri ya Kiislamu ya Iran
Akizungumza katika mapokezi ya msafara huo wa operesheni ya mabaharia 44 wa meli za jeshi uliopewa jina la Matumaini ya Golestan, amezungumzia mahusiano ya kistratijia baina ya Iran na Afrika Kusini na kusema kuwa, misafara hiyo ni yenye umuhimu wa aina yake kwa ajili ya kuinua kiwango cha stratijia baina ya nchi mbili. Msafara wa meli za kundi la 44 la kikosi cha baharini cha jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na ambazo hapo awali zilitia nanga jijini Dar es Salaam, Tanzania, ulianza mwanzoni mwa mwezi Oktoba mwaka huu kwa kupitia maji ya kimataifa ya Ghuba ya Aden na langobahari la kistratijia la Bab-el-Mandeb.
Moja ya meli za kibiashara zinazolindwa na meli za kijeshi za Iran
Jukumu la msafara huo ni kudhamini usalama wa meli za kibiashara na mafuta za Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kutokana na vitisho vyovyote vya baharini dhidi yake. Aidha imeelezwa kuwa, hatua hiyo inalenga kuwafikishia ujumbe wa amani na urafiki watu wa Afrika Kusini. 

0 comments: