MASHAMBULIO YA NDEGE ZA KIVITA ZA SAUDIA YAENDELEA KUUA RAIA WA YEMEN
Posted by khamisimussa77@gmail.com at 12:18 AM
Watu 19 wameuawa katika mashambulio mapya ya
anga yaliyofanywa na ndege za kivita za Saudi Arabia dhidi ya maeneo ya
makaazi ya raia nchini Yemen.
Watu 16 wameuawa na wengine 11 wamejeruhiwa wakati ndege za
kivita za Saudia ziliposhambulia mji wa Murawa'ah mkoani Al Hudaydah
magharibi mwa Yemen.
Ndege za kivita za jeshi la utawala wa Aal Saud zimeshambulia pia mji wa Ad-Durayhami na kuua raia watatu.
Wakati huohuo jeshi la Yemen likishirikiana na vikosi vya kujitolea
vya wananchi vimejibu jinai na mashambulio hayo ya wavamizi kwa
kushambulia kwa makombora ngome za jeshi la Saudia katika maeneo ya
Jizan, Najran na Usair na kufanikiwa kuwaangamiza askari kadhaa wa jeshi
hilo.
Kikosi cha makombora cha jeshi la Yemen na wapiganaji wa kujitolea
kimeshambulia pia boti za kivita za muungano vamizi wa kijeshi
unaoongozwa na Saudia katika pwani ya mji wa Dhabab mkoani Taiz kusini
magharibi mwa Yemen na kusababisha hasara kubwa kwa boti hizo.
Aidha ndege moja isiyo na rubani (drone) ya vikosi vamizi vya Saudia
ilianguka jana usiku karibu na uwanja wa ndege wa kimataifa wa Aden
kusini mwa Yemen.../
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: